Tangakumekuchablog
Tanga, JUMLA ya
watoto wanne wamezaliwa katika mkesha wa Sikukuu ya Pasaka katika kituo cha
Afya Ngamiani Tanga ikiwa ni pungufu ya
idadi kama hiyo mwaka jana.
Akizungumza na waandishi wa habari,
Muuguzi wa zamu kituo cha afya cha Ngamiani, Vestina Paul, alisema kati ya
watoto hao wawili ni wa kike na wawili ni wakiume.
Alisema wazazi wote walijifungua
salama na watoto wao wakiwa katika afya nzuri na kudai kuwa awali walitegemea
idadi ya wajawazito kujifungua ingeongezeka na hivyo wauguzi walikuwa
wamejipanga kupokea waliotaka kujifungua.
“Mara nyingi mikesha ya Sikukuu iwe
ya Pasaka au Iddi kituo huwa kinaongeza nguvu zaidi ya kupokea
wajawazito----hii ikiwa ni kuhakikisha wajawazito wanajifungua salama na kuweza
kusherehekea sikukuu kama wengine” alisema Paul
“Jambo zuri ambalo hatukutegemea
tumezalisha watoto wanne----hii ni idadi pungufu ya mwaka jana na ndio maana
tulijipanga kwa kutegema kuongezeka” alisema
Wakati akizungumza na wazazi wa
watoto hao, Muuguzi huyo aliwataka kuwa mabalozi wazuri katika maeneo yao kwa
kutoa elimu ya wajawazito kuwa na ada ya
kutembelea vituo vya afya kujua mwenendo wa ujauzito wao.
Alisema kuna wajawazito wengi
wamekuwa hawana ada ya kufika katika vituo vya afya na badala yake wamekuwa wakienda wakati
wanapojisikia uchungu na hivyo kuwa kero.
“Wajawazito wengi hawana elimu ya
kutembelea vituo vya afya kujua mwenendo wa ujauzito wao----hii inapelekea mara
nyingi mzazi kukumbana na changamoto wakati wa kujifungua” alisema Paul
Alitoa ushauri kwa wazazi hao kuhakikisha
wanakuwa mabalozi wazuri mitaani ikiwa na pamoja na kupiga vita mimba za
utotoni pamoja na vitendo vya ukatili wa wanawake na watoto.
Mwisho
No comments:
Post a Comment