Simba Vs Yanga: Tambwe, Omog wa kwanza kushuka Taifa
Yanga ilikuwa ya kwanza kuingia uwanjani 8:30 mchana na mchezaji wa kwanza kushuka alikuwa Amissi Tambwe akifuatiwa na Obrey Chirwa na meneja na wengi walirusubili kwa sekunde kadhaa nao wakashuka wa mwisho alikuwa kocha Hans Pluijm na msaidizi wake Juma Mwambusi.
Yanga kwa kuwa ni wenyeji waliingia kukaa vyumba vya upande wa kushoto ambao umezoeleka na kuwa wa Simba.
Simba iliingia uwanjani saa 8:40 mchana wa kwanza kushuka alikuwa kocha Joseph Omog akifutiwa na Jackson Mayanja, huku nahodha Jonas Mkude alikuwa wa kwanza kwa wachezaji.
Makomandoo wa Simba wanampiga mtoa huduma ya kwanza kwa madai alikuwa akipuliza dawa kwenye vyumba vyao.
Baada ya kulindima mabomu ya machozi ya kuwatawanya mashabiki waliokuwa wakifanya vurugu, hatimaye TFF na wasimamizi wa uwanja walikubaliana kutumika kwa kadi za selcom pekee kuruhusu mashabiki kuingia uwanjani hapo.
Baada ya uamuzi huo mashabiki walitulia na kurudi katika mistari yao ya kuingia uwanjani kwa kuonyesha kadi na kuingia uwanjani.
No comments:
Post a Comment