MAJONZI TELE! FAMILIA YALAZWA NJE!
Familia hiyo ikiwa nje baada ya nyumba yao kuvunjwa. Stori: Deogratius Mongela na Chande Abdallah
Familia moja yenye makazi yake Mtaa wa Mwembe-Madafu, Ukonga jijini
Dar, imejikuta ikihamishia makazi yake nje kwa madai kwamba
nyumba yao imevunjwa na baada ya kuuzwa kwa mtu mwingine na mwanafamilia
anayetajwa kwa jina la Omary Hamisi ambaye ni mtoto mkubwa wa familia
hiyo.
Akizungumza kwa masikitiko makubwa mbele ya vyanzo vya habari mmoja wa
wanafamilia hao, Rajabu Hamisi (28) alisema kuwa historia ya nyumba hiyo
ilianzia pale baba yao, Hamis Mangandali alipopewa na mzee mmoja
aliyemtaja kwa jina la moja la Kombo mwaka 1961.
Rajabu alisema kwamba, migogoro ilianza mwaka 1991 baada ya Bibi
Kombo Mbwana (mmoja wa wanafamilia ya Kombo) alipomkabidhi nyumba hiyo
baba yake, Hassani Ali aliyetajwa kama babu yao mzaa mama. Alisema kuwa
babu huyo aliiuza nyumba hiyo kwa mtoto huyo mkubwa wa mzee Hamisi
aitwaye Omari Hamisi kwa kiasi cha shilingi elfu sabini (70,000/=) bila
wanafamilia wengine kufahamu.Rajabu aliongeza kwamba, mwaka 2012,
familia yao ilishangaa kupokea notisi ikiwataka wahame nyumba hiyo kwa
muda wa siku 14 kwa kuwa ilikuwa tayari imeuzwa.
Baadhi ya vitu vya familia hiyo vikiwa nje. “Tulishangaa lakini hatukuwa na namna. Tuliendelea kuishi kwenye nyumba.
“Kweli baada ya siku kutimia walifika watu wakatutupia virago nje.
“Walipoondoka tukarudisha vitu ndani na kuendelea kuishi lakini kwa
wasiwasi,” alisema Rajabu ambaye alidai kuwa sekeseke hilo lilijitokeza
mwanzoni mwa mwezi huu hadi sasa.Alisema ukiachilia mbali kutupiwa vitu
nje, nyumba hiyo ilivunjwa kabisa huku ndugu yao aliyedaiwa kuiuza
akitowekea kusikojulikana.
“Hadi sasa familia yetu yote ipo nje, si watoto wala baba wote
tunakaa nje, mvua yetu, jua letu. Kimsingi sisi hatuna cha sikukuu wala
nini,” alisema Rajabu na kuongeza kuwa kwa kipindi chote hicho wamekuwa
hawamuelewi ndugu yao ambaye ameuza nyumba hiyo kuwa ana nia gani na
familia yao hasa baba yao ambaye ni mzee.
Familia hiyo inaomba mtu yeyote aliyeguswa na matatizo yao aisaidie
kwa hali mali kupitia namba 0688 35 44 44 0752 26 41 27 kwa kuwa haina
msaada wowote.
No comments:
Post a Comment