Kumekucha blog
Tanga, JAMII imetakiwa kuwapa malezi mazuri watoto wao pamoja na kuwabidiisha katika elimu ili kuwa
msaada katika maisha yao ya baadae na kusisitiza kuwa kutofanya hivyo ni
vigumu maendeleo kupatikana.
Akizungumza wakati wa kutoa zawadi kwa watoto sherehe
ya Krismass leo, Mchungaji Manasse Maganga wa kanisa la Glory Land Church sabasaba, alisema jamii iko na jukumu la kuwalea watoto katika
malezi ya kiucha Mungu.
Alisema kuna wimbi la watoto wa mitaani wanaozagaa na
kudai kuwa wote ni kukosa elimu na
malezi ya wazazi wao na hivyo kujingiza katika magenge ya ombaomba na watumiaji wa madawa
ya kulevya.
Alisema ili kuifanya jamii kuishi katika maisha bora
na furaha ni wajibu wa kila mzazi na mlezi kuwangalia watoto na kuwafundisha
maisha ya kiroho jambo litakaloweza kusaidia kuwa na familia za watoto wenye
tabia nzuri.
“Leo ni siku ya furaha na tupo hapa kwa lengo moja tu
la kuzaliwa kwa Yesu Kristo---furaha hii iwe ni kichocheo cha kusonga mbele
katika mambo ya elimu na afya” alisema
Maganga na kuongeza
“Zawadi hizi tunazowapatia vijana wetu ni kutokana na
wao kuonyesha ukaribu na maisha ya roho mtakatifu----naomba iwe chachu ya hatua
mbili mbele katika maendeleo na huduma za kijamii” alisema
Akizungumzia kuhusu
hali ya amani na utulivu uliopo, mchungaji Manasse amewataka viongozi wa
madhehebu ya dini kuwahubiria waumini wao juu usalama uliopo.
Alisema usalama na amani uliopo sio wa kuchezewa jambo
ambalo ukitoweka kuurejesha tena vigumu na hivyo kuwataka kila mmoja kusisitiza
watu kuisha kwa pamoja na mshikamano.
Wakati wa sherehe hiyo, mchungaji huyo wa kanisa la
Glory Land Church alitoa zawadi mbalimbali kwa watoto na makundi ya watu ikiwa
ni furaha ya Sikukuu kwa kila mmoja kufurahi na kusameheana.
Mwisho
No comments:
Post a Comment