Maswali
hayo yanatokana na maazimio ya Bunge ambayo yalionekana kuvuta hisia za
wananchi katika kona mbalimbali za nchi ambako walikuwa wanafuatilia
moja kwa moja mjadala wa Bunge hadi kupitishwa maazimio hayo.
Hotuba
hiyo inayotarajiwa kutolewa wakati Rais atakapozungumza na wazee wa Dar
es Salaam, ikiwa ni siku nne baada ya Kampuni za IPTL na Pan Africa
Power Solutions (PAP) kukimbilia mahakamani kuzuia utekelezwaji wa
maazimio ya Bunge.
Baadhi ya
wasomi nchini wamesema hatua ya kuzuia utekelezaji wa maazimio hayo
pamoja na kauli ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,
Profesa Anna Tibaijuka kuwa akijiuzulu Rais atamshangaa, ni mambo
yanayofanya hotuba ya Rais kusubiriwa kwa hamu.
Swali la
kwanza ambalo wananchi wanasubiri jibu lake ni iwapo Rais Kikwete
atatuliza kiu yao kuhusu kashfa hiyo ambayo imekuwa gumzo nchi nzima na
hivyo kulegeza msimamo wa wahisani wa kuinyima nchi misaada.
Pili,
wananchi wanasubiri kusikia iwapo Rais Kikwete ataagiza uchunguzi zaidi
wa Takukuru, Polisi na vyombo vingine kama ambavyo azimio la kwanza la
Bunge linavyotaka wahusika wachukuliwe hatua za kisheria kuhusika na
vitendo vyote vya kijinai kuhusiana na miamala ya Akaunti ya Tegeta
Escrow.(MM)
Tatu,
wanasubiri kwa hamu kuona hatua ambayo Rais Kikwete atachukua dhidi ya
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, Katibu Mkuu wa
wizara hiyo, Eliakim Maswi pamoja na Profesa Tibaijuka kutokana na
kutajwa katika maazimio hayo ya Bunge.
Kwa
nyakati tofauti, viongozi hao wamekaririwa wakisema kuwa hawahusiki na
kashfa hiyo. Mbali ya Profesa Tibaijuka kujitokeza kujitetea mwenyewe,
baadhi ya wananchi wamejitokeza kuwatetea na kuwasafisha viongozi hao
katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.
Nne, Je,
atatengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Umeme (Tanesco)
ambayo pia ilitakiwa kuwajibishwa ikiwa chini ya Mkuu wa Majeshi
mstaafu, Jenerali Robert Mboma.
Tano, ili
kuwachukulia hatua majaji waliotajwa, Aloysius Mujulizi na Profesa
Eudes Ruhangisa, Rais Kikwete anatakiwa aunde Tume ya Kijaji ya
kuchunguza tuhuma za utovu wa maadili zinazowakabili, kinachosubiriwa
kwa hamu ni kuona endapo ataunda tume hiyo.
Swali la
sita linalohitaji jibu linahusu kupambana na kudhibiti vitendo vya
rushwa kubwa, ufisadi na hujuma za uchumi. Kinachosubiriwa ni jibu la
Rais Kikwete iwapo Serikali itaandaa na kuwasilisha muswada wa
marekebisho ya sheria iliyoiunda Takukuru kwa lengo la kuanzisha taasisi
mahsusi itakayoshughulikia masuala hayo.
Vilevile,
wananchi wanatazamia kupata suluhisho la gharama kubwa za umeme katika
jibu la Rais Kikwete iwapo Serikali iko tayari kuinunua mitambo ya
Kampuni ya IPTL kama ilivyopendekezwa na Bunge kwa lengo la kuokoa fedha
za Tanesco zinazotumika kununua umeme kwa bei ya juu.
WANANCHI
No comments:
Post a Comment