Kumekucha blog
Tanga, WATOTO 11 wamezaliwa katika hospitali
ya rufaa ya Bombo Tanga, wakiwemo mapacha wa kike na kiume waliozaliwa kwa njia
ya uperesheni na kuifanya idadi hiyo
kuwa pungufu na mwaka jana.
Muuguzi wa zamu wodi ya wazazi, Ashirina Mwanyoka,
alisema kati ya idadi hiyo wanaume ni 7 na wa kike 4 ambapo mama mmoja,Suzana
Petro kujifungua watoto pacha wa kike na wa kiume.
Alisema idadi hiyo ni pungufu ya watoto waliozaliwa
mwaka jana jambo ambalo halikuleta shida baada ya wauguzi kujipanga kukabiliana
na wazazi wanaojifungua kutokana na wahudumu kujumuika na familia zao
kusherehekea Krismass.
“Hakukuwa na shida yoyote kwani mbali ya kuwa tulikuwa
tayari kukabiliana na wajawazito ambao wako tayari kujifungua---kama unavyojua
kuwa vipindi vya sikukuu tunakuwa na upungufu mdogo” alisema Mwanyoka
“Jambo ambalo tunaweza kusema ni la kufurahisha na
kujivunia mkesha wa krismass ni kuwa
tumepata pacha wa kike na wakiume ambao wamezaliwa kwa operesheni wakiwa salama
na afya njema” alisema
Akizungumzia wajawazito kuhudhuria vituo vya afya
kabla ya kujifungua, Mwanyoka alisema kuna baadhi yao wamekuwa wakifika
hospitali wakati wa kujisikia uchungu na hivyo wauguzi kupata wakati mgumu.
Alisema hali hiyo
inawapa shida ya kutojua maendeleo ya ujauzito pamoja na vipimo hivyo kuwataka kufuata ushauri wa madaktari lengo
likiwa ni mzazi kujifungua katika mazingira ya usalama na mtoto wake.
“Kama mjamzito hana utaratibu wa kuhudhuria kliniki
kwa kweli sisi wauguzi tunakuwa katika mazingira magumu----mtu anakuja hana
damu na hana rikodi za maendeleo ya ujauzito wake” alisema Mwanyoka
Alisema ili mzazi kuepuka matatizo wakati wa
kujifungua amewataka wajawazito kuwa na ada ya kufika vituo vya afya mara kwa
mara ikiwa ni faida yake na mtoto na kuwa msaada kwa wauguzi.
No comments:
Post a Comment