Thursday, December 25, 2014

SOMA MKUSANYIKO WA STORI ZA MAGAZITI YA LEO,TZ

Nimekuwekea hapa mkusanyiko wa Story kubwa tano kutoka kwenye Magazeti ya leo December 25

MKUSANYIKO HUU UNALETWA KWENU NA MKOMBOZI SANITARIUM CLINIC MABINGWA WA MAGONJWA SUGU, WAPO CHUDA TANGA

Nimekuwekea hapa mkusanyiko wa Story kubwa tano kutoka kwenye Magazeti ya leo December 25

News (1)MWANANCHI
Kesi ya kuchoma moto bendera ya CCM inayomkabili Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari jana imeahirishwa mpaka January 20, 2015 kutokana na Hakimu David Mwita kuwa safarini.
Mbunge huyo pia hakuhudhuria kesi hiyo kwa kuwa alikuwa safarini, kesi hiyo inatokana na tuhuma anazokabiliwa nazo za kuchoma bendera ya CCM yenye thamani ya sh. 250,000/- iliyokuwa mali ya Raphael Moses, yuko huru kwa dhamana ya watu watatu ya sh. Mil.1.5.
 MWANANCHI
Hakimu Godfrey Haule wa Mahakama ya Mwanzo Mirerani , Manyara amegoma kumwapisha mshindi wa nafasi ya uenyekiti Mbuki Mollel kwa madai kuwa ushindi wake una utata na kuongeza kuwa atazua mgogoro kwenye jamii.
Hakimu huyo amesema zoezi la kumwapisha Mwenyekiti huyo litafanyika muda wowote baada ya Mahakama kujiridhisha na ushindi wa Mollel.
Desemba 14 wakazi wa Kijiji cha Kambi ya Choka walimsimika Joshua Kuney kuwa mwenyekiti wao wakidai kwenye kura za maoni CCM ndiye waliyemchagua kwa kura 335 dhidi ya Mollel 215, huku Mbuki akisema kuwa yeye ndiye Mwenyekiti halali.
NIPASHE
Wajawazito Wilaya ya Chato wameiomba Serikali Wilayani humo kutunga Sheria ndogondogo  za kuwataka wanawake kujifungulia vituo vya kutolea tiba na kuwabana wanaume kuhudhuria kliniki ili kupunguza vifo vinavyotokana na uzazi.
Takwimu za WHO zinaonyesha takribani wajawazito 79,000 hufariki kila mwaka nchini huku kukiwana wastani wa vifo 22 kila siku.
Kumekuwa na mapokeo tofauti kwa wananchi juu ya elimu ya uzazi wa mpango ambapo wapo wanaoamini kutumia njia za uzazi wa mpango ni kupingana na agizo la Mungu, wengine wakisema ni shinikizo la nchi za Ulaya zenye lengo la kurudi kuitawala Afrika na wengine wakiamini kuwa huo ni mpango wa kupunguza idadi ya watu kinyume cha mila na desturi.
Mganga Mkuu Hospitali ya Wilaya ya Chato amesema Serikali na asasi mbalimbali bado zina jukumu la kutoa elimu kwa wananchi ili wabadili mtazamo wao kuhusu uzaziwa mpango.
 MTANZANIA
Majambazi wamevamia duka na kupora fedha kiasi cha mil. 4.5 na kumuua kwa kumpiga risasi kichwani Gloria Marandu maeneo ya Kinondoni, Dar ambaye alikuwa anapita njia.
Kamanda wa Polisi Camillus Wambura amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema wahusika wa tukio hilo hawajakamatwa lakini upelelezi unaendelea.
Wambura amewataka wananchi kutoa taarifa na ushirikiano pale wanapoona kuna viashiria vya uvunjifu wa amani.
 JAMBO LEO
Ofisa mwandamizi wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi Tarime, PC Degratias amejeruhiwa kwa kuchomwa na mkuki ubavuni na wavamiziwa mgodi wa Acacia North Mara walioingia kuokota mawe ambayo yalidhaniwa kuwa na dhahabu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tarime, Lazaro Mambosasa amesema askari huyo alijeruhiwa juzi saa saba mchana alipokuwa kwenye operesheni ndani ya mgodi huo akiendesha gari ambapo kundi la watu hao walivamia gari aliyokuwa akiendesha na kumjeruhi.
Askari huyo amelazwa Hospitali ya Halmashauri ya Tarime akipatiwa matibabu huku Polisi wakiendelea na upelelezi wa watuhumiwa waliohusika na tukio hilo.
Nakuhakikishia kwamba nitakufikishia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia,kumekucha blog

No comments:

Post a Comment