Tuesday, January 20, 2015

ZAMBIA YAFANYA UCHAGUZI MKUU, LEO

Zambia kwenye uchaguzi mkuu leo, pichaz na story yote hapa

cq5dam.web.540.390Leo wananchi wa Zambia wanapiga kura kuchagua Rais wa nchi hiyo, baada ya kufariki kwa liyekuwa Rais wa nchi hiyo,  Michael Sata ambaye alifariki mwezi October, 2014 akiwa kwenye matibabu  London, Uingereza.
Chama tawala cha Patriotic Front kinawakilishwa na Edgar Lungu na  Hakainde Hichilema anayewakilisha United Party for National Development kwenye uchaguzi huo.
Election II
Tume ya Uchaguzi Zambia imesema zoezi la kuhesabu kura litaanza muda mfupi baada ya kukamilika kwa zoezi la kupiga kura na matokeo yatatangazwa ndani ya saa 48, Rais atakayeshinda atakaa madarakani kwa kipindi cha miezi 18 tu ili ufanyike uchaguzi mkuu mwingine.
Election
Hakuna story itakayokupita mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia,tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment