Labda password yako ni moja kati ya hizi zilizovunja rekodi mwaka 2015… Zicheki hapa!
Hivi
karibuni tumesikia watu wengi wakiwemo wasanii wakilamika juu ya
account zao pamoja na simu kuvamiwa na wezi wa mitandaoni, watafiti
wanasema matumizi ya password dhaifu pia huchangia account hizo
kuvamiwa, au wengine kutumia password moja kwenye account zaidi ya moja
ikiwemo email, simu na mitandao ya kijamii.
Utafiti uliofanywa na kampuni ya SplashData,
Marekani umeonyesha kuwa password milioni 3.3 zilizotumika mwaka 2014
katika maeneo ya Amerika ya Kaskazini na Ulaya Magharibi zilivuja huku
majina kama Michael, Thomas, Andrew na Daniel yakionekana kuwa majina yanayotumiwa sana kwenye password.
Takwimu hiyo imeonyesha kuwa password nyingi ambazo zinatumika zimekuwa ni rahisi sana kiasi kwamba zinawapa urahisi hackers kuzitabiria na kuweza kuvamia account hizo kirahisi na kushauriwa password nzuri ni ya kuchanganya namba na tarakimu.
Utafiti huo umetoa password 25 zilizotumiwa na watu wengi duniani kwa mwaka 2014, ambazo ni 2.2% ya password zote.
Hii ni list ya password hizo 25 ambazo zimetumika zaidi 2014.:: 123456
:: password
:: 12345
:: 12345678
:: qwerty
:: 1234567890
:: baseball
:: dragon
:: football
:: 1234567
:: monkey
:: letmein
:: abc123
:: 111111
:: mustang
:: access
:: shadow
:: master
:: michael
:: superman
:: 696969
:: 123123
:: batman
:: trustno1
Nitafurahi kusikia kutoka kwako mtu wangu, vipi hapo ipo ambayo uliwahi kutumia?
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia,tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment