Thursday, August 11, 2016

TANZANIA YAKWEA NAFASI MOJA VIWANGO VYA FIFA

Tanzania yashuka viwango vya FIFA

Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), Agosti, 11 limetoa orodha ya timu zinaoongoza kwa ubora duniani na nchi ya Argentina ikiendelea kusalia kileleni ikiwa na alama 1585.

Nafasi ya pili inashikwa na Ubelgiji, nafasi ya tatu Colombia, nafasi ya nne Ujerumani na nafasi ya tano ikishikiliwa na Chile.

Kwa upande wa Tanzania imeshuka kwa nafasi moja kutoka nafasi ya 123 hadi nafasi ya 124 na kwa Afrika Mashariki ikishika nafasi ya 5, nyuma ya Uganda, Kenya, Rwanda na Burundi.

Aidha viwango hivyo vimeonyesha kuwa kwa Afrika, Algeria inaongoza ikifuatiwa na Ghana, Ivory Coast na Senegal ikishika nafasi ya nne

No comments:

Post a Comment