SIMULIZI ZA FAKI A FAKI 0655 340572
MWANAMKE 55
ILIPOISHIA
Baba yake Abdi alikufa wakati
Abdi akiwa mkubwa. Huyo baba yake ndiye aliyekuwa na ile pete aliyokuwa anavaa
Abdi. Abdi aliichukua siku baba yake alipokufa akaivaa yeye bila kujua maana
yake.
Kwa vile Abdi ni mpenda ushirikina alikuwa mganga wake mzee mmoja
mrefu ambaye alimwambia kuwa ile pete ni ya jini mwanamke ambaye alikuwa mke wa
babu yake aliyekufa zamani huko Tanga.
Abdi akaambiwa kwamba kama atampata jini huyo na atamuoa na yeye atakuwa
tajiri. Hapo ndipo Abdi alipopata kichaa. Akaanza kufanya makafara ya kumvuta
huyo jini lakini ilishindikana.
Akaambiwa na mganga, kwa vile
yeye ameshaoa mke, huyo jini hawezi kumpata kwani jini huyo haendi kwa mtu
mwenye mke wake. Asubiri kama mke wake atakufa ndio huyo jini anaweza kumpata.
Abdi akaona hakuwa na sababu
ya kumtaliki mke wake akamtilia sumu kwenye chakula ili afe. Baada ya kumuua
mke wake akarudi tena kwa yule mganga. Akafanyiwa makafara lakini huyo jini
hakutokea.
Safari hii akaambiwa kwamba
huyo jini tayari ana mtu mwingine na mtu huyo ni ndugu yake aliyeko Tanga,
yaani mwana wa baba yake mdogo.
Akaambiwa ndugu yake huyo
anaitwa Umari au Amiri au Amour na nyota yake ni Nge.
SASA ENDELEA
Shamsa aliendelea kunieleza
kuwa mganga alimwambia Abdi kuwa dalili ya kumtambua huyo ndugu yake ni kuwa
anapokabiliwa na hatari jini wake anajigeuza joka kubwa na kuwashambulia watu
wanaotaka kumdhuru huyo ndugu yake.
Siku moja wakati Abdi yuko
kwenye boti yake akifuatilia pembe zake za ndovu kutoka Tanzania, alielezwa na nahodha wa boti iliyotoka
Tanzania
kuhusu mkasa uliowafika ambapo baada ya kumkamata mtu waliyemdhania kuwa ni
mpelelezi likatokea joka ambalo liliwaua wenzake.
Abdi aliposikia mkasa huo
akayakumbuka yale maneno ya mganga wake kwamba huyo ndugu yake mwenye huyo
jini, jini wake hujigeuza joka.
Shamsa alinieleza wazi kuwa
mimi ni ndugu yake Abdi na jini anayemtaka Abdi ni Zena.
Siku ile nilipokutana na Abdi
kwenye ile boti, Abdi aliniambia.
“Wewe unaitwa Umar au Amiri
au Amour”
Nikamwambia ninaitwa Amour.
Akajua ndio mimi mwenye huyo
jini aliyekuwa anamtaka. Maelezo ya Shamsa yalinifanya nigundue sababu ya Abdi
kunichukua kwa nguvu huko Somalia.
Mganga wake pia
nilishamfahamu, alikuwa ni yule mzee mrefu wa kisomali.
Kumbe ndiyo maana yule mzee
alinifuata usiku akanichukua pale hoteli kimiujiza na kunipeleka katika shimo.
Kumbe alikuwa ananifanyia uganga wa
kumpata Zena!
Halafu siku ile Abdi alinipeleka
kwa yule mganga ambaye alifanya makafara yake mpaka Zena akatokea na kumpiga
kofi, mimi na Abdi tukakimbia. Kumbe zile zilikuwa jitihada za kumpata Zena!
Shamsa alinieleza kuwa mganga
alishindwa kumchomeka Zena kwa Abdi na hivyo walibuni mpango mwingine.
Mpango huo ulikuwa ni wa
kuniua mimi kikatili. Abdi aliambiwa anikamate na kunining’iniza kichwa chini
kisha atoboe utosi wangu kwa msumari.
Damu itakapotoka aikinge kwenye kikombe cheupe kisha ajipake yeye kwenye utosi
wake ili aweze kumpata Zena.
“Shamsa umeijuaje habari yote
hii?” nikamuuliza Shamsa baada ya kunieleza mkasa huo.
“Hii ni habari ya siri,
usimwambie Abdi na wala usiniulize nimeijuaje isipokuwa mtahadhari Abdi. Abdi
ni ndugu yako lakini ni mshenzi. Au utakataa kwamba huna baba yako mdogo
aliyepotea baharini miaka ya nyuma.?”
“Yupo. Niliambiwa kuwa
alipotea baharini lakini mimi nilikuwa mdogo au sijazaliwa”
“Basi ndiyo hivyo”
“Siku zote nilikuwa
ninajiuliza kwanini Abdi amenileta hapa Somalia kwa nguvu, kwanini ananiita
ndugu yake na kwanini alilitambua jina langu mara tu baada ya kuniona. Kumbe
kuna vitu vilivyojificha nyuma ya pazia
“Pia nilikuwa nikijiuliza
kwanini alinipeleka kwa yule mganga na kwanini Zena alitokea na kumpiga kibao…”
“Amekubali apate gharama za
kukuweka wewe hapa Somalia,
lengo lake ni
hilo”
“Nashukuru kwa kunifahamisha.
Sasa unanishauri nifanye nini?”
“Endelea kumuangalia tu,
jifanye kama hujui lolote”
“Si anataka kuniua?”
“Huo mpango wao bado, siku
watakayotaka kufanya hivyo nitakwambia”
“Mh! Kwa kweli umenitia
hofu!”
“Una maana kwamba huniamini
mimi mke wako?” Shamsa akaniuliza.
“Ninakuamini” nikamjibu.
“Kama
unaniamini endelea kuniskiliza mimi na fuata vile ambavyo nitakwambia”
“Sawa. Lakini ninataka kujua wewe umejuaje habari zote hizo?”
“Mimi niko karibu sana na Abdi”
“Na kuhusu upande wa baba
yangu mdogo aliyekuja huku Somalia
umejuaje habari zake?”
“Hakuna kisichofahamika
Amour. Au ulikuwa hutaki miye mke wako nijue habari zako?”
“Hapana. Ukijua habari zangu
ni vizuri kwa sababu mimi ni mume wako”
“Sasa tulia. Endelea na kazi
yako kama kawaida, zungumza na kaka yako Abdi
bila uoga, siku ya watakayopanga kufanya ushenzi wao nitakwambia siku moja
kabla na nitakupa mbinu ya kufanya”
“Nakushukuru sana mke wangu kwa kunizindua. Umejibu maswali yangu mengi
niliyokuwa nikijiuliza bila kupata majibu. Ninaamini kuwa wewe ni mke wangu wa
kweli”
“Na mimi nakushukuru sana mume wangu kwa
kunisikiza na kuniamini. Wewe utakuwa mume wangu wa kudumu”
“Asante
sana”
Shamsa alitabasamu kisha
akanipiga busu kwenye shavu langu.
“Hebu niambie ilikuwaje siku
ile kwenye ile boti wakati wale jamaa walipotaka kukutosa?” akaniuliza.
Nikamueleza Shamsa
ilivyokuwa.
“Lilipotokea hilo joka na kuwazamisha
hao waliotaka kukutosa, wewe ulifikiri nini?” akaniuliza.
“Leo ndio nimepata jibu
kutoka kwako. Hilo swali nilikuwa nikijiuliza sana. Nilikuwa sijui ni
kwanini lile joka linetokea na lilitoka wapi. Kumbe ni jini linalonifuata mimi”
“Kumbe wewe siku zote
tunaishi lakini kulikuwa na kitu unanificha!”
“Kitu gani?”
“Kwamba una jini wa kike
mwenye utajiri”
“Kwa kweli niliogopa kukutia
hofu. Huyu jini mimi simtaki na amekuwa akinifanyia vituko vingi sana mpaka nimekimbia huko
kwetu…”
MAMBO NDIYO HAYO. JE NINI
KITATOKEA? TUKUTANE KESHO
No comments:
Post a Comment