Shindano la Miss Tanzania limefungiwa. Taarifa kamili ipo hapa.
Tangu atangazwe aliyekuwa Miss Tanzania 2014 Sitti Mtemvu
mengi yameongelewa kuhusiana na tetesi za udanganyifu wa umri na vitu
vingine kadhaa vinavyomhusu mrembo huyo ikiwemo suala la umri wake na
kiwango cha elimu yake ambapo yeye mwenyewe alikanusha taarifa hizo.
Story ikaendelea Novemba 8, 2014 siku
ambayo Kamati ya Miss Tanzania ilikutana na waandishi wa habari Dar es
salaam na kutangaza kwamba Sitti Mtemvu ameandika barua kwa hiari yake yeye mwenyewe, kwamba amelivua taji hilo hivyo kamati hiyo ikamtangaza Lilian Kamazima aliyekuwa mshindi wa pili kushikilia taji hilo.
Leo December 25 kuna taarifa kwamba
Serikali imelifungia shindano la Miss Tanzania kwa miaka miwili kutokana
na sababu mbalimbali na ukiukwaji wa taratibu walizojiwekea, ikiwemo
udanganyifu mkubwa unaojitokeza kila mwaka kwenye shidano hilo.
Maamuzi hayo yamechukuliwa na BASATA, ambapo Kaimu Mtendaji wa Baraza hilo Godfrey Mngereza
amesema maamuzi hayo yalifikiwa baada ya kukaa kikao cha tathmini
ambapo Kamati ya Miss Tanzania ilishindwa kujibu hoja za msingi za wadau
na kukiri kuwepo udhaifu katika uendeshaji wa shindano hilo.
“Baada
ya kupitia maelezo yote na taarifa ya tathmini ya shindano hilo ni
vyema tulisimamishe kwa muda ili mwandaaji ajipange upya, atakaporejea
arejee kwa nguvu na kuandaa shindano lenye hadhi kubwa kuliko ilivyo
hivi sasa…“– Mngereza.
Shindano hilo limekumbwa na kashfa mbalimbali tangu mwaka 2006 ikiwemo ya kuvisha mataji warembo wasiokidhi vigezo.
Chanzo cha Habari: Gazeti la Mtanzania, December 25.
Nakuhakikishia kwamba nitakufikishia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia, kumekucha blog
No comments:
Post a Comment