Pale ambapo Askari walitumia mabomu machozi kuwatawanya watoto walioandamana Kenya
Askari Polisi wa Kenya katika mji mkuu Nairobi leo wamewafyatulia mabomu ya machozi wanafunzi wa shule ya msingi Lang’ata waliokuwa wakiandamana kupinga kunyang’anywa ardhi ambayo ilikuwa kiwanja chao cha michezo.
Polisi hao wakiwa na mbwa waliwatawanya
wanafunzi ambao wengi wao inasemekana kuwa watoto wenye umri wa miaka
sita baada ya kuangusha ukuta mpya uliojengwa katika eneo la shule.
Baadhi yao walipelekewa hospitalini
baada ya kupata majeraha madogo madogo huku polisi mmoja akiumizwa baada
ya kupigwa jiwe usoni na wanafunzi.
Hii imetokea leo January 19, siku ambayo
wanafunzi hao walifika shule kwa mara ya kwanza baada ya mgomo wa
walimu uliokuwepo kwa wiki mbili kutokana na madai yao ya mishahara.
Taarifa hii unaweza kuitazama hapa, hii nimekutolea kituo cha K24 Kenya.
Hakuna Story itakayokupita mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia,tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment