Bush kuiongoza Marekani kama rais kwa mara nyingine.
Gavana wa zamani wa Jimbo la Florida nchini Marekani Jeb Bush ametangaza kujiuzulu mnafasi mbalimbali ambazo anashika kwenye makampuni kadhaa pamoja na nyadhifa anazoshika kwenye bodi za taasisi mbalimbali zisizo za kibiashara ikiwa ni ishara ya dhamira ya gavana huyo wa zamani ya kuingia moja kwa moja kwenye mbio za kuwania urais katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwaka 2016 .
Kwa mujibu wa msaidizi wa karibu wa mwanasiasa huyo , Jeb ambaye ni mdogo wa rais wa zamani wa Marekani George Walker Bush ataangalia uhusiano alio nao kwneye biashara tofauti katika kipindi cha mwaka mwaka huu akiwa na lengo la kujiondoa kwenye biashara na kuingia kikamilifu kwneye siasa akiwania nafasi ya kukiwakilisha chama cha Republican kwenye uchaguzi wa mwakani .
Jeb Bush alitangaza mwishoni mwa mwaka 2014 kuwa anafuatilia kwa karibu mchakato wa urais japo hajaweka wazi azma yake ya kuingia kwenye mbio hizo .
Jeb Bush anatarajiwa kutangaza azma ya kuwania urais wa Marekani katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2016.
Msemaji wa Jeb pia amethibitisha kuwa Jeb ataendelea kubaki kwenye bodi za makampuni ambayo yeye ni mshirika ikiwemo kampuni yake ya usharui wa masuala ya biashara ya Jeb Bush anad Associates .
Tayari Bush alishajiuzulu kwenye bodi ya wakurugenzi kwenye kampuni za Rayonier Inc , Tenet Healthcare Corporation na benki ya Uingereza ya Barclays .
Rais
wa zamani wa Marekani Mzee George Herbert Walker Bush (kushoto) na rais
mwingine wa zamani wa Marekani George Walker Bush (katikati) na Jeb
Bush (kulia) katika picha ya pamoja .
No comments:
Post a Comment