Hekaheka ya leo Jan 19 iko hapa inamhusu msichana aliyepelekwa Oman kufanya kazi za ndani.
Kwenye Hekaheka ya leo Jan 19 inatokea
Dar inamhusu Binti mmoja aliyepelekwa Oman na mtu aliyemfahamu kwa ajili
ya kufanya kazi za ndani, lakini hakuwa na maisha mazuri kutokana na
manyanyaso makubwa aliyoyapata kwa bosi wake ambaye ni mtanzania
anayeishi huko.
Baada ya kufanya kazi kwa wiki mbili
yalianza manyanyaso kutoka kwa bosi wake na familia yake ikiwemo vitisho
vya kuuwawa, alipoomba arejeshwe nyumbani walimkatalia, akaamua
kutoroka.
Njiani alikutana na mtu aliyemsaidia
kwenda kituo cha Polisi na baada ya maelezo bosi wake alipigiwa simu na
kufika kituoni kutoa maelezo, wakafikia muafaka wa binti huyo kurudi kwa
bosi wake kuendelea na kazi.
Aliporudi manyanyaso yalizidi ikiwemo
bosi huyo kuwaamuru watoto wake kumdhalilisha na kumnyima mshahara,
alijifanya kachanganyikiwa kwa kuanza kupiga kelele, bosi wake akaamua
kumkatia tiketi ili arudi nyumbani bila kumpa hela yoyote.
No comments:
Post a Comment