Ndugu wa marehemu wameukosa mwili wa mtu wao, kaburi halikuachwa wazi!
Mwili wa mtu aliyeuawa na mamba katika
Ziwa Baringo, Kenya mwezi December inasemekana umezikwa bila idhini ya
familia ya mtu huyo.
“Inatolewa
inapelekwa mahali pengine ambayo hata hatujui ni ajabu sana… Sisi
tumesema tunataka mwili wa mtoto wetu, tunataka mwili wa mtoto wetu mara
moja” alisema ndugu wa marehemu.
Familia hiyo iliandaa kaburi la kumzika
ndugu yao lakini ikashindikana kutokana na mwili wake kukosekana katika
chumba cha kuhifadhia maiti ambapo inasemekana kuwa baada ya Polisi
kufika katika eneo ambalo mtu huyo aliuawa na mamba, waliwaamrisha ndugu
zake wasiufuate mwili huo kwa kuwa walikuwa wakiupeleka kuufanyia
upasuaji ili kuweza kubaini kifo chake, lakini baadaye ndugu walipokea
taarifa ya ndugu yao kuzikwa kwenye kaburi la siri.
“Mpaka
sasa wazee wakasema okay chukueni miti ili ipresent huo mwili, ukiletwa
inatolewa, hatuwezi kuchimba kaburi bila mtu… hii kaburi atakula watu
sasa kwetu” alisema ndugu mwingine wa marehemu.
Familia hiyo imeitaka Serikali kuingilia kati ishu hiyo na kueleza nani aliyetoa maamuzi ya kuuzika mwili wa ndugu yao.
No comments:
Post a Comment