Arsenal yaondokewa na mshambuliaji wake.
Klabu ya Arsenal imemruhusu mshambuliaji wake Lukas Podolski kujiunga na mabingwa wa zamani wa ulaya Inter Milan zikiwa zimepita siku chache tangu kocha wa Arsenal Arsene Wenger akanushe taarifa za mshambuliaji huyo kuondoka.
Podolski anajiunga na Inter baada ya kushindwa kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha Arsenal ambapo mara nyingi amejikuta akiwa mshambuliaji wa akiba ambaye mara zote amekuwa akitokea benchi pamoja na kuwa na rekodi nzuri ya kufunga kulingana na nafasi ndogo anayopewa.
Lukas Podolski ameondoka Arsenal na kujiunga na Inter Milan baada ya kukosa nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza.
Siku chache zilizopita kocha wa Arsenal Arsene Wenger alikanusha taarifa za kuondoka kwa Podolski baada ya kuulizwa na waandishi wa habari ambapo jibu la kocha huyo mfaransa lilikuwa ‘hapana Podolski hataondoka’.
No comments:
Post a Comment