Thursday, January 1, 2015

SOMA HABARI KUU KATIKA MAGAZETI YA LEO, TZ

Mkusanyiko wa Stori zilizopewa Headlines kwenye Magazeti ya leo Tanzania January 1, 2015

Mkusanyiko wa Stori zilizopewa Headlines kwenye Magazeti ya leo Tanzania January 1, 2015

januuuTANZANIA DAIMA
Mbunge wa Kigoma  Kusini David Kafulila amesema kuwa mwaka 2015 ni mgumu kwani Serikali ipo taabani kifedha kiasi cha kusitisha kandarasi ya barabara kutokana na ukata.
Alisema Mamlaka ya Mapato Tanzania wanakusanya bilioni 800 kwa mwezi wakati mahitaji ya mishahara pekee ni takribani bilioni 500 na kwamba kiasi cha bilioni 300 kinachosalia hakitoshi hata kununua karatasi na mafuta ya kuendesha ofisi za Serikali nchi nzima.
Alisema Serikali iko katika hali mbaya wakati iko kwenye kutaka kutekeleza mambo makubwa yanayohitaji fedha uku mwaka huu ukiwa ni wa uchaguzi ambao ni muhimu kwa nchi yoyote duniani.
MTANZANIA
Hali si shwari ndani ya chama cha Alliance for Change ACT baada ya kuwafukuza uanachama aliyekua Katibu mkuu wake Samson Mwigambana mshauri wa chama hicho Profesa Kitila Mkumbo.
Mbali na hao viongozi wengine waliovuliwa nyadhifa zao ni pamoja na aliyekua Makamu Mwenyekiti bara Shabaan Mambo,Mwenyekiti wa Wazee Wilson Muchumbusi na katibu wa vijana Philip Malaki.
Mwenyekiti wa ACT Kadawi Lukas alisema  uamuzi huo umefikiwa baada ya kuitishwa kikao cha kamati kuu kilichofanyika jana.
Tumewavua uongozo na kuwafukuza uanachama Kitila na Mwigamba kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ya kutumia madaraka vibaya kwa kukabidhi chama kwa mafisadi.
Alisema viongozi hao walisaini makubaliano ya kuendesha shughuli za chama  ikiwemo kusimamia mikutano na uchaguzi bila kushirikisha viongozi wengine.
NIPASHE
Ulazaji wa bomba la maji la Mamlaka ya majisafi na majitaka Dar es salaam Dawasa katika mradi wa Ruvu chini kuanzia Bagamoyo hadi Dar umekamilika kwa asilimia 93.
Mradi huo unatarajiwa kukamilika March na utakua ukitoa maji lita milioni 270 kwa siku katika maeneo mbalimbali ya Jiji na sehemu ambazo bomba linapita.
Dawasa imesema kuwa mradi huo umefikia hatua hiyo baada ya jitihada za  kutatua mgogoro huo  kwa kuzungumza na wakazi ambao bomba hilo linapita ambao walifungua kesi mahakamani kuupinga wakidai walipwe fidia.
Menejamradi huo Romanus Mwangingo alisema kuwa mradi huo unatazamiwa kukamilika baada ya kulaza bomba katika maeneo yote.
NIPASHE
Mbunge waviti maalum kupitia UVCCM Mkoa wa Arusha Catherine Magige amelalamikiwa kwa kuwagombanisha viongozi wa Jumuiya ya wanawake UWT Mkoa wa Arusha  kutokana na kinachodaiwa kuwa ni mbio zake za ubunge kupitia Jumuiya hiyo.
Mgongano huo unadaiwa kutokana na ukiukwaji wa kanuni  kilichofanywa na Mbunge huyo kwa kugawa zawadiza vitenge na mchele kwa ajili ya sikukuu za Krismass kwa viongozi wa Jumuiya hiyo bila kuutaarifu uongozi wa juu.
Pia kamati hiyo imemfungia ofisi Katibu wake Stamil Dendegu kwa tuhuma za kumruhusu Magige kugawa zawadi na kumkaimisha  ofisi katibu wa UWT Wilaya ya Arusha Fatma Hassan.
Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Arusha Flora Zelote alikanusha kusimamishwa kazi kwa katibu wake wala kuwepo kwa kikao kilichomjadili yeye.
NIPASHE
Siku chache baada ya Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu kutangaza nia ya kuwania Urais, Sheikh Shariff Matongo ameibuka na kusema mmoja wa viongozi anayewania nafasi hiyo ya juu atafariki dunia.
Sheikh Shariff alitoa utabiri huo  juu ya ndoto zilizomjia usiku na kuoteshwa mambo zaidi ya matano yatakayoikabili nchi mwaka huu.
Alisema atakayefariki dunia ni yule mgombea anayewania nafasi ya urais ambaye alishawahi kuwa kiongozi katika nyadhifa mbalimbali kupitia CCM.
Ndoto yangu nilioteshwa sikukaa nayo peke yangu niliwaeleza Masheikh mbalimbali kutoka Abu Dhabi, Nigeria na kupata ushauri wao na wakaniambia suala hilo nisikae nalo bali niwashirikishe Watanzania wenzangu“alisema.
MWANANCHI
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge yahesabu za Serikali Zitto Kabwe amesema atamuunga mkono kiongozi wa kambi ya upinzani Freeman Mbowe pale atakapowasilisha hoja yake bungeni kuhusu ufisadi wa zaidi ya trilioni 1 katika mradi wa bomba la gesi kutoka Mtwara kwenda Dar es salaam.
Najua bado mnalia kuhusu bombala kupeleka gesi Dar es salaam,machozi yenu yatafutika kwani tayari habari ya ufisadi mkubwa katika ujenzi wa bomba hilo zimeanza kuchomoza.”Zitto.
Kiongozi wa Upinzani Mbowe ametamka mara kadhaa kuwa atatoa hoja kuhusu ufisadi kuhusu ujenzi wa bomba hilo,na pale atakapohitaji msaada wetu tutamsaidia,tunaamini gharama za mradi huu zimezishwa mara mbili na inawezekana kabisa kuwa zaidi ya dola milioni 600 sawa na zaidi ya trilion 1“alisema Zitto.
Alisema katika miakaya hivi karibuni Mkoa wa Mtwara umechukua sura mpya baada ya kugundulika kuwa na gesi na wananchi wameonekana kuwa wanaweza kupigania maslahi ya Taila lao.
MWANANCHI
Timu ya Makachero wa Polisi kutoka Dar es salaam imewasili Mwanza kuongeza nguvu za kumsaka mtoto mlemavu wa ngozi Pendo Emmanuel anyesadikiwa kutekwa akiwa nyumbani kwao.
Polisi wametangaza dau la milioni 3 kwa atakayewezesha kutoa taarifa za waliohusika kufanya tukio hilo la kumteka mtoto huyo.
Hata hivyo taarifa zilipatikana jana zinasema tayari watu sita wameshikiliwa na polisi wakishusishwa na tukio hilo akiwemo baba wa mtoto huyo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Valentino Mlowola  ataiongoza timu hiyo inayowashirikisha pia Makachero wa Mkoani Mwanza kuhakikisha mtoto huyo anapatikana aidha akiwa amekufa ama akiwa hai.
Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia,kumekucha blog

No comments:

Post a Comment