Irom Sharmila: Mgomo mrefu zaidi wa njaa kumalizika
Mwanaharakati nchini India Irom Sharmila anakamilisha mgomo wake wa kukataa chakula dhidi ya sheria tata baada ya miaka 16.
Mwanaharakati
huyo anatarajia kuanza kula hii leo baada ya mahakama katika jimbo la
kaskazini mashariki mwa nchi hiyo la Manipur kumuachilia huru leo.
Amekua
katika mahabusu ya mahakama na kulazimishwa kula kupitia mrija kupitia
pua lake kuepuka sheria inayoadhibu uhalifu wa kutaka kujiua.
Lakini mwezi uliopita aliiambia mahakama kwamba anataka kukatiza mgomo
wake na kuanza kampeni yake kama mgomea huru katika uchaguzi ujao wa
wabunge .
Bi Sharmila amekua akipinga sheria inayopatia jeshi
mamlaka maalum (AFSPA), ambayo inawapatia wanajeshi mamlaka yote ya
kuwakamata watu bila vibali na hata kupiga risasi kwa lengo la kuua
katika majimbo kadhaa nchini India , likiwemo jimbo la Manipur na la
Kashmir.
Mpiga picha Ian Thomas Jansen-Lonnquist alifuatilia kwa karibu safari yake katika miaka michache iliyopita. Ameishi kipindi kirefu cha miaka 16 chini ya
uangalizi wa mahakama katika hospitali ya ya mji mkuu wa jimbo la
Manipur, Imphal,ambako alilazimishwa kunywa mchanganyiko wa madawa na
maziwa ya unga ya watoto wachanga Bi Sharmila aliachiliwa huru mwezi Agosti 2014
baada ya mahakama kukataa shitaka kwamba "anajaribu kukujiua ". Lakini
alikamatwa tena siku mbili baadae baada ya kukataa kumaliza mgomo
wake. Bi Sharmila alikuwa akihudhuria mahakama kuu ya Manipur kila baada ya wiki mbili kurejelea msimamo wake mgomo. Mgomo wake wa chakula ulitambuliwa kote duniani,
ambapo shirika la haki za binadamu la Amnesty International
lilimuelezea kama mfungwa mwenye mawazo huru. Mwanaharakati huyo alivivutia vyombo vya habari vya ndani ya nchi na vya kimataifa katika miaka ya hivi karibuni . Bi Sharmila alikua na ufuasi wa wanawake na makundi yanayopigania haki za kijamii katika jimboni. Makumbusho yamejengwa katika eneo la Manipur
ambako raia 10 waliuliwa na wanajeshi wa India. Jimbo hilo lina jumla ya
wakazi milioni 2.5 na kikosi kikubwa cha wanajeshi , na polisi wengi
walipelekwa huko kukabiliana na makundi ya waasi.
No comments:
Post a Comment