Wakazi wa Zahrau Ngamiani Tanga wakiangalia pikipiki ambayo imenasa chini ya Uvungu wa Coastal ambayo ilitambulia kwa jina kama la SHASHUI ambayo hufanya safari yake Tanga Lushoto.
Katika ajali hiyo ambayo mashuhuda walisema dereva wa pikipiki alikuwa mwendo kasi na kushindwa kukata kona na kupelekea kuserereka na pikipiki yake kuingia chini ya Uvungu na dereva wa pikipiki kunusurika kifo.
Dereva huyo ambaye hakutambulika jina lake alikimbizwa hospitali ya Bombo kwa matibabu baada ya kupata Mstuko na Michubuko mwilini.
Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo ameiambia tangakumekuchablog kuwa heko na sifa zote ziende kwa dereva wa Coastal kwa umahiri wake baada ya kumkwepa dereva wa pikipiki na kusalimika kifo.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment