Swansea yakata dau la Everton
Timu ya soka ya Swansea City imekataa dau la pauni milioni 10 lilitolewa na Everton ili kuweza kumsajili beki Ashley Williams.
Taarifa
zinasema beki huyo raia wa Wales ambae pia ni nahodha wa Swansea alikua
anakaribia kufika makubaliano ya mwisho kwenda Goodison Park kujiunga
na Everton.Williams ambae atafikisha miaka 32 mwezi huu anamkataba na timu yake unaomalizika mwaka 2018, msemaji wa klabu hiyo anasema hawako tayari kumuuza beki huyo.
Everton wanasaka saini ya beki huyu ili kwenda kuziba pengo litakaloachawa na mlinzi wao mahiri John Stones anayehusishwa kutaka kujiunga na matajiri wa Man City.
No comments:
Post a Comment