Mfalme Akihito wa Japan aomba kung’atuka
Mfalme wa Japan Akihito ameeleza mapenzi yake ya kutaka kung'atuka.
Akihutubia
taifa hilo kupitia runinga, amesema ana wasiwasi kwamba umri na udhoofu
wa afya yake huenda vikamfanya ashindwe kutekeleza majukumu yake.Kwa sasa, hakuna nafasi kisheria kumruhusu mfalme kuondoka madarakani Japan.
Lakini muda mfupi baada ya hotuba yake, Waziri Mkuu wa Japan, Shinzo Abe, amesema atathmini kwa makini ombi la mfalme huyo.
Mfalme Akihito amekuwa madarakani tangu kifo cha baba yake, Hirohito, mwaka 1989.
Habari kwamba anataka kung'atuka zilianza kutokea kwenye vyombo vya habari mwezi jana.
No comments:
Post a Comment