Saturday, September 10, 2016

MFEREJI WA MAJI MACHAFU MASIWANI UMEKUWA KERO SUGU

 Mfereji wa maji taka barabara ya 12 Masiwani Tanga  karibu na Kanisa na makazi ya watu ukiwa na maji yaliyotuwaa na kuzusha hofu ya kitisho cha kuzuka kwa magonjwa ya miripuko na mazalia ya mbu.
Mfereji huo ambao wakazi wengi wanaoishi jirani mtaro huo wamesema kuwa ile Dhamira ya Serikali kukomesha malaria inaweza kusuasua kama hakutakuwa na hatua za dharura za kukabiliana na mazingira ya utunzaji usafi mitaani.
Wakazi hao wameiambia tangakumekucha kuwa Halmashauri ya jiji inatakiwa kutoa agizo zito kwa wenyeviti na watendaji kata kusimamia na kutoa adhabu kwa wanakaidi kuweka mazingira ya usafi maeneo yao.



No comments:

Post a Comment