Sunday, September 11, 2016

IBADA YA HIJJA YAFIKIA KILELE MECCA

Ibada ya Hajj yafika kilele chake mlima Arafat

Mahujaji wakongamana katika mlima Arafat huku baadhi yao wakisoma Quran
Ibada ya Hajj nchini Saudia imefika kilele chake huku takriban Waislamu milioni 1.5 wakikongamana katika mlima Arafat ili kufanya maombi ya siku nzima mbali na kusoma Quran.
Mahujaji hao walikongamana katika mlima huo wakati wa macheo ambao uko takriban kilomita 15 kutoka mji wa Mecca.
Waislamu wanaamini kwamba mtume Muhammad alitoa hotuba yake ya mwisho katika eneo hilo.
Nguzo ya Hajj ni mojawapo ya nguzo tano za kiislamu ambayo Waislamu hutakiwa kuitekeleza ijapokuwa mara moja.
Siku ya Jumamosi ilibainika kuwa kiongozi mkuu wa dini nchini Saudia Abdul Aziz al-Sheikh hakuweza kutoa hotuba yake ya kawaida kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 35 kutokana na matatizo ya kiafya.

No comments:

Post a Comment