Uchunguzi umebainisha kuwa dhana ya
kuwa asili ya binadamu wa kwanza ni kutoka Afrika ya Mashariki zaidi ya
miaka laki mbili iliyopita sio kweli.
Visukuku vya binadamu watano imepatikana Kaskazini mwa Afrika na inaonyesha binadamu wa
kwanza aliishi miaka 100,000 zaidi ya vile ilivyodhaniwa. Prof Jean-Jacques Hublin, kutoka Leipzig, Ujerumani, anasema kuwa ugunduzi huu unaweza "kuandika upya vitabu vya kiada" kuhusu kuibuka kwetu .
"Sio hadithi ya hayo kutokea kwa njia ya haraka katika 'shamba la Edeni' mahali fulani barani Afrika. Ilikuwa ni maendeleo ya taratibu. Kwa hiyo kama kulikuwa na bustani ya Edeni, ilikuwa ni kote kote Afrika.
BBC
No comments:
Post a Comment