Pochi na matumizi yake, huyu aliitumia hivi…
Wanyama
kama mbwa na paka wamekuwa wakithaminiwa sana na watu wa Ulaya,
Marekani na kuna wakati unakuta mtu anambeba paka au mbwa wake kwenye
pochi au begi kwenda naye matembezini.
Lakini hii ya mama huyu inatoka China, Xue Hsueh amewashangaza
watu wengine kumchukulia kama mnyanyasaji na katili, yeye aliamua
kumbeba mtoto wake wa miezi tisa katika pochi yake.
Alipiga picha huku mwanaye huyo akiwa kwenye pochi na kuisambaza kwenye mitandao, comment
za watu wengi walimkosoa wakionyesha kuchukizwa na kitendo hicho japo
alijitetea kwa kusema alimuweka mtoto huyo kwenye pochi kwa muda mfupi
na kumtoa, picha hiyo alipiga kuwatania marafiki zake.
Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia,kumekucha blog
No comments:
Post a Comment