Haya ni maamuzi ya Steve Gerrard baada ya msimu huu wa Ligi kuisha…
Nahodha huyo wa zamani wa England, Steven Gerrard anamaliza mkataba wake na klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu na amechukua uamuzi wa kutoongeza mkataba mpya.
Liverpool walimpa ofa mpya Gerrard
mwezi November mwaka jana lakini kiungo huyo mwenye miaka 34 alifikia
uamuzi wa kutaka kwenda sehemu nyingine kupata changamoto mpya.
Katika taarifa rasmi iliyotolewa na klabu ya Liverpool Steven Gerrard amesema;”Nimeamua
kutangaza uamuzi huu sasa ili kocha na timu isipoteze umakini kwenye
mambo ya msingi kutokana na tetesi juu ya hatma yangu.“
“Liverpool
Football Club ni sehemu kubwa ya maisha yangu na jambo hili la kuondoka
hapa ni uamuzi mgumu zaidi niliowahi kufanya katika maisha yangu,
lakini ni uamuzi ambao utakuwa na faida kwa watu wote wanaohusika,
ikiwemo familia yangu na klabu yenyewe.”– Gerrard.
‘Nitaendelea
kucheza soka lakini siwezi kuthibitisha wapi nitaenda baada ya kutoka
hapa, ila kwa uhakika kabisa haitokuwa hapa nikimaanisha sitoichezea
klabu ambayo itakuwa na upinzani au itacheza dhidi ya Liverpool – hilo
ni jambo ambalo nawaahidi mashabikiwa Liverpool.” – Gerrard.
Gerrard alianza rasmi kuitumikia Liverpool mwaka
1998, mpaka sasa anatajwa kuwa mmoja ya wachezaji bora kabisa wa muda
wote wa klabu hiyo akiwa ameichezea mechi 695 na kufunga magoli 177.
Haya hapa ni makombe ambayo amewahi kutwaa akiwa na Liverpool.
Champions League -2
FA Cups- 2
League Cups- 2
UEFA Cup- 2
UEFA Super Cups- 2
Charity Shield- 2
No comments:
Post a Comment