Wednesday, October 14, 2015

UTOVU WA NIDHAMU WAMPOZA JOSE MOURINHO

Utovu wa nidhamu wamponza Mourinho, hii ndio adhabu inayomkabili…

Chama cha soka cha England FA, kimempa adhabu kocha wa klabu ya Chelsea Jose Mourinho kutokana na utovu wa nidhamu.
Mourinho amepewa adhabu ya kulipa Faini ya dola 75,000 sawa na zaidi ya fedha za kitanzania milioni 150 pamoja na kufungiwa mchezo mmoja huku  FA wakiangalia mwenendo wake.
Meneja huyo wa Chelsea alimshambulia kwa maneno mwamuzi Robert Madley aliyechezesha mchezo wao dhidi ya timu ya Southampton baada ya kuchapwa kwa mabao 3-1
Mourinho alikasirishwa na Refa Madley kutowapa Penati na kudai Waamuzi wanaogopa kutoa uamuzi kwa Timu yake.
Kauli hiyo iliwafanya FA wamfungulie Mashitaka ya Utovu wa Nidhamu wakidai kauli za Mourinho zinalenga zinazochochea vurugu.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment