Monday, October 12, 2015

DJOKOVIC ANYAKUA TAJI TENA

Staa huyu wa Tennis duniani katika ushindi mwingine…


Mcheza tenesi namba moja kwa ubora duniani kwa upande wa wanaume Novak Djokovic ametwaa taji la michuano ya wazi China.
Djokovic alimshinda mpinzani wake Rafael Nadal anayeshikilia nafasi ya nane kwa ubora wa mchezo huo duniani kwa Seti 6-2 6-2 ikiwa ni ushindi wa taji lake la sita kwa mwaka huu.
Kwa upande wa wanawake Garbine Muguruza kutoka hispania alipata ushindi wa seti 7-5 6-4 dhidi ya Timea Bacsinszky na kutwaa taji la pili.
Ushindi huo unamfanya Muguruza kupanda hadi nafasi ya nne kwa ubora wa viwango vya mchezo huo.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment