Wednesday, October 14, 2015

SOKA NA SUTI UWANJANI, UMEWAHI KUONA?

Kuanzia sasa hivi, wakali wa Arsenal ni mwendo wa suti tu wanapoingia uwanjani..!!

Klabu ya Arsenal ya Uingereza ambayo inafundishwa na kocha raia wa Ufaransa Arsene Wenger, October 14 wachezaji wa timu hiyo wameingia kwenye headlines za mitandao ya kijamii baada ya kuonekana wamevaa suti huku wakioneshana ufundi wa kuchezea mpira.
2
Suti hizo nyeusi ambazo wamevaa wachezaji hao zinaonekana kuwa za kufanana na kwa haraka ukiwaona utatamani ujue kuna sherehe inayofanya nyota hao kuvaa suti zinazofanana? Ripoti kutoka mirror.co.uk inasema kampuni ya nguo za kiume ya Duchamp London imeidhamini klabu ya Arsenal.
3
Duchamp London ambayo inajihusisha na utengenezaji wa suti hizo inatajwa kuingia mkataba na Arsenal, hivyo itakuwa inawavalisha wachezaji wa Arsenal, makocha na viongozi wa klabu hiyo wakiwa katika mechi au katika sherehe mbalimbali zitakazokuwa zinahusisha wachezaji na viongozi wa klabu hiyo.
f
1 n
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment