Tutegemee kumuona Chicharito Arsenal January? msikie mkurugenzi wa Bayer Leverkusen …
Mshambuliaji wa kimataifa wa Mexico ambaye amewahi kuichezea klabu ya Man United kwa miaka kadhaa Javier Hernandez Chicharito kabla ya mwaka 2015 kuamua kujiunga na klabu ya Bayer Leverkusen ya Ujerumani, amekuwa akihusishwa kuhitajika na klabu ya Arsenal ya Uingereza.
January 3 mkurugenzi wa michezo wa klabu hiyo Rudi Voller ameongelea uwezekano wa mchezaji huo kuondoka ndani ya Leverkusen
ni mdogo sana hususani ukizingatia wapo katikati ya msimu, hivyo ni
ngumu kwa wao kumuacha aondoke. Jibu hilo linakuwa pigo kwa Arsenal
ambao wanatajwa kuwa walikuwa na imani ya kumpata.
“Chicharito
ana nafasi kubwa sana ndani ya kikosi chetu, hususani kwa aina yake ya
ushambuliaji na ndio maana tukamsajili katika timu yetu, ndio kwanza
tupo katikati ya msimu na kila kitu kinaenda sawa ni rahisi kukataa ofa
za vilabu vingine” >>> Rudi Voller
Kauli ya Rudi Voller inalenga kuvikatisha tamaa vilabu vya Ulaya ambavyo vimekuwa vikivutiwa na huduma ya mmexico huyo. Chachiroto hadi sasa amefunga magoli 11 katika michezo 1 aliyocheza katika Ligi Kuu Ujerumani.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment