Zimevuja jezi mpya za Man City za msimu wa 2016/2017, rangi yake kuwashangaza wengi, cheki hapa …
Imekuwa ni kawaida kwa vilabu vya soka
vya Ulaya ila mwaka kubadili aina ya jezi kwa ajili ya msimu mpya, lengo
kubwa la kubadili aina ya jezi huwa inatajwa kuwa ni namna ya
kutengeneza mauzo ya jezi na kuongezea mapato kwa klabu. January 5 footy headlines imetangaza kuvuja kwa aina ya jezi za ugenini watakazo vaa klabu ya Manchester City kwa msimu wa 2016/2017.
Jezi hizo mpya za Man City zinatajwa kuvuja na zitakuwa na rangi ya machungwa na zikichanganyika na rangi ya zambalau, hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa Man City kuvaa jezi zenye rangi ya machungwa kwa mechi za ugenini toka wafanye hivyo msimu wa 2008/2009.
Jezi hizo mpya ambazo zitakuwa za tatu kwa Man City zinatajwa kuzinduliwa mwezi September, lakini bado hawajaonesha rasmi picha ya jezi hizo zaidi ya kuvuja kwa Logo na Nike na Etihad wataendelea kuwa wadhamini wa Man City
kama kawaida. Rangi ya jezi hizo inatajwa kuja kuwashangaza wengi
kutokana na uwepo wa rangi ya machungwa ambayo mara ya mwisho kuvaliwa
ilikuwa miaka nane nyuma.
No comments:
Post a Comment