Baada ya Chelsea kupitia kipindi kigumu, Terry ana haya, Fabregas na Pedro muda wa kupiga self umepatikana …
Klabu ya soka ya Chelsea January 3 ilivunja mwiko wa kutopata matokeo mazuri kwa kuiadhibu klabu ya Crystal Palace kwa jumla ya goli 3-0 katika uwanja wa ugenini. Chelsea
ambayo ilikuwa katika wakati mgumu kwa kupoteza mechi nyingi kuliko
kawaida yake, wachezaji wameanza kuwa na furaha na matokeo hayo.
Nahodha wa klabu hiyo John Terry amefunguka na kuanza kujivuna kuwa hiyo ndio Chelse ya mwaka uliopita imeanza kurudi, wakati Pedro na Fabregas wameonesha matabasamu yao katika mitandao ya kijamii. Terry anaamini wameanza kurejea katika hali yao ya kawaida kama ambavyo alisema Guus Hiddink kocha wa muda wa Chelsea.
“Hii
sasa naweza sema ni kama Chelsea ya msimu uliopita imeanza kurudi,
michezo ndio tunaipa kipaumbele lakini sifikirii kama huu ndio mwisho wa
kupata matokeo mazuri. Mwaka mpya, tumeanza vizuri na tunalazimka
kuendelea na ushindi kwa kila mechi. Kocha mpya amaekuja na inaonekana
ameanza kuimarisha kiwango cha kila mmoja kama ilivyokuwa awali”
>>> John Terry
Kwa habari, matukio na michezo ni hapa hapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment