Tangakumekuchablog
Tanga, JESHI la Polisi
Mkoani hapa limewauwa watu wawili wanaodhaniwa kuwa majambazi kwa kuwapiga
risasi wakati wa majibizano ya risasi kwenye
msitu wa Pongwe nje kidogo ya jiji la Tanga.
Majambazi hao ambayo kwa mujibu wa
Kamanda wa Polisi Tanga, Leonard Poul, amesema kwa wiki mmoja mfululizo
walikuwa wakifanya uporaji kwenye maduka makubwa na Raia wa kigeni.
Akizungumza na vyombo vya habari
ofisini kwake, kamanda Poul amesema utupianaji wa risasi ulianzia mjini Tanga baada ya majambazi hayo kukimbia baada ya
kufanya uporaji wao kwa kutumia pikipiki.
Kamanda amewapongeza waendesha
pikipiki maarufu kama Bodaboda kwa ushirikiano wao kwa kushiriki kikamilifu
kuwafukuza majambazi hayo hadi kwenye msitu wa Pongwe na kufanikiwa kuwauwa.
Amesema kuuwawa kwa majambazi hayo
kulitokana na kuishiwa kwa risasi walizokuwa na nazo na badala yake kujificha
kwa kupanda katika miti na wakati wa msako huo walionekana wakiparamia juu ya
miti.
Mwisho
Kamanda wa polisi Mkoani Tanga, Leonard Poul, akiwaonyesha waandishi wa habari dawa ambayo vibaka wamekuwa wakiitumia kupuliza katika madirisha ya nyumba usiku na kwenye vioo vya magari na ambavyo hulainisha na kuweza kuiba kwa urahisi.
Kamanda wa polisi Mkoani Tanga, Leonard Poul, akiwaonyesha waandishi wa habari kioo cha gari kilichopakwa dawa na kulainika na wizi kufungua mlango na kuiba vitu vilivyokuwemo ndani.
Mwalimu wa shule ya msingi ya Pongwe halmashauri ya jiji la Tanga, Dominica Tarimo akizungumza na waandisi baada ya watu wanaoaminika kuwa waizi kupaka dawa kwenye kioo cha gari yake kiliolainisha na kuweza kufungua mlango na kuiba vitu vyote vilivyokuwemo ndani.
No comments:
Post a Comment