Wanajeshi wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) wakishiriki kufanya usafi kituo cha Afya Cha Makorora Tanga leo.
Jeshi hilo limefanya usafi maeneo mbalimbali ya jiji la Tanga na baadhi ya watu wamelipongeza kwa hatua yake hiyo hali ambayo jiji limebadilika na kuwa katika hali ya usafi.
Said Nassou mkazi wa Makorora alisema hatua hiyo iwe endelevu hatua ambayo itaondosha na kutokomeza magonjwa ya miripuko na malaria yanayosababishwa na mazalia ya mbua kwa uchafu.
Amewataka wananchi kuiga mfano huo wa kila siku kufanya usafi na kuacha kusubiri tarehe za usafi za kitaifa.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment