Friday, November 3, 2017

RIWAYA, KAMA UNATAKA FEDHA ZA MAJINI, SEHEMU YA 14

RIWAYA

KAMA UNATAKA FEDHA ZA MAJINI 14

ILIPOISHIA

Kwa vile yule Maalim aliniambia niseme shida yangu, nikazungumza kwa sauti ya kusikika kile kilichokuwa moyoni mwangu. Nilieleza kwamba baba yangu ambaye kwa wakati ule ni marehemu alifika mahali hapo na kutaka apate pesa za majini.

Nikaendelea kueleza kwamba marehemu  alipatiwa mke wa kijini  na alipata utajiri kama alivyotaka lakini inasemekana alinitaja mimi kama mrithi wake bila kunishauri mwenyewe.

“Sasa baba mwenyewe amekufa, yule jini pamoja na zile pesa za majini vimekuja kwangu. Kilichonileta hapa ni kuwa mimi sizitaki zile pesa kwa sababu siye niliyeziomba na pia simtaki yule mke wa kijini, nataka arudi kwao” nikasema.

Lakini sikuishia hapo tu, niliendelea kuzungumza kuwa baba alimtoa kafara mke wake pamoja na mjukuu wake ambaye ni mwanangu mimi ili kutimiza masharti ya kupata utajiri.

“Sasa nataka mama yangu pamoja na mwanangu wawe wazima kama zamani. Na pia yule jini ameniambia kuwa mke wangu naye atatolewa kafara. Mimi sitaki atolewe kafara kwa sababu sitaki utajiri wa pesa zile” nikasema.

Nikamalizia kwa kueleza.

“Kwa hiyo nataka yule jini arudi kwao na zile pesa zirudi huku huku na mama yangu na mwanangu wawe wazima”

Nilipomaliza nilisubiri kwa dakika moja, sikuona kitu chochote. Nikageka na kurudi kwa wale watu.


SASA ENDELEA


“Enhe, umeambiwa nini?” Maalim akaniuliza.

Nikatikisa kichwa.

“Sikuambiwa kitu”

“Lakini umefanya kama nilivyokuagiza?”

“Ndiyo. Nilipofika nimeeleza shida yangu kama ulivyoniambia”

“Ulitangulia kumuita mwenyewe?”

“Mwenyewe nani?”

“Maimuna binti Ibilisi. Nilikwambia ukifika umuite mara tatu halafu kitatokea kivuli ndio utakiambia shida yako”

“Loh…nilisahau. Sikumuita Maimuna na wala sikukiona hicho kivuli”

“Sasa hizo shida ulimwambia nani?”

“Nilijisemea tu”

“Umekosea, rudi tena”

“Duh!”

Nikageuka na kuutazama tena ule mti.

“Inakubidi uende tena ukaseme kama nilivyokuagiza” Maalim akaniambia.

“Sawa”

Nikageuka tena na kuanza mwendo.

Nilipofika pale mahali niliposimama mara ya kwanza, niliita jina la Maimuna binti Ibilisi mara tatu.

Nikakiona hicho kivuli kama cha mwanandamu kimetokea mbele ya ule mti.

Kisha nikasikia sauti laini ya mwanamke ikiniitikia.

Kwa sababu nilishituka kutokana na kukiona kivuli hicho na kusikia ile sauti ya mwanandamu ikivuma, nilitaka kukimbia lakini kwa vile ni tukio ambalo nilikwishaambiwa kuwa litatokea, nikajikaza. Sikukimbia.

“Wewe ni nani” Ile sauti ikaniuliza.

Nikakumbuka kujitaja jina langu.

“Unatoka wapi?”

Nikajieleza.

“Eleza shida yako”

Nikaanza kueleza kama nilivyoeleza mara ya kwanza.

Nilipomaliza maelezo yangu, ile sauti ikaniuliza.

“Baba yako alikuwa naitwa nani?”

Nikataja jina lake.

“Alifika lini hapa?”

“Kwa kweli, siwezi kujua. Ilikuwa ni siri yake”

“Je ni mali gani ambayo umemrithi?”

“Ni nyumba na sanduku la pesa”

“Na kitu gani kingine?”

“Ni nyumba na pesa tu”

“Wewe unaishi kwenye nyumba gani?”

“Kwa sasa ninaishi kwenye nyumba hiyo hiyo”

“Umetumia kiasi gani kwenye hizo pesa ulizorithi?”

“Sijatumia hata senti moja”

Pakapita ukimya wa karibu dakika moja. Kile kivuli bado kilikuwa pale pale. Sikuelewa maana ya ukimya ule. Kwa vile Maalim aliniambia kuna majibu ambayo nitapewa, ikabidi niendelee kusubiri.

Ghafla ile sauti ikaniuliza.

“Umesema hutaki utajiri?”

“Siutaki” nikajibu.

“Na humtaki yule mwanamke wa kijini?”

“Ndiyo, simtaki”

Pakapita ukimya mwingine wa kama nusu dakika kabla ya ile sauti kusikika tena.

“Umekubaliwa lakini mama yako na mwanao watapotea”

Kauli ile ilinipa taharuki nikajikuta nikiuliza.

“Kwanini wapotee?”

“Kwa sababu baba yako alishatumia zile pesa, inabidi kafara litoke” Sauti hiyo ikaniambia.

“Mama yangu!” nikang’aka na kujaribu kumtetea mama yangu na mwanangu.

“Lakini mimi ninazirudisha hizo pesa na sijazitumia, wale watu si wangeachiwa tu wakaendelea na maisha yao”

“Hii ndio kanuni yetu, haiwezi kubadilika” Ile sauti ikaniambia.

“Hakuna njia nyingine ya kufanya ili mama yangu na mwanangu wasalimike?”

“Kazungumze na Maalim halafu yeye ataniambia mimi kama atakubali”

“Basi nitakwenda kuzungumza naye nimsikilize ataniambia nini”

Niliposema hivyo kile kivuli kikatoweka. Nikageuka nyuma na kuondoka.

Nilitembea kwa mwendo wa haraka haraka kuelekea kule walikosimama Maalim na mwenzake.

Nilipofika Maalim aliniuliza.

“Je mmekubalianaje?”

“Ameniambia kwamba nimekubaliwa ila mama yangu na wanangu watapotea”

“Sawa. Sasa jibu umeshalipata, kutakapokucha urudi kwenu”

“Sasa kulikuwa na suala moja”

“Suala gani?”

“Kuhusu mama yangu na mwanangu ambao baba aliwatoa kafara ili apate zile pesa”

“Wana nini?”

“Nilitaka nao waachiwe wawe wazima”

“Sasa hayo ungeyaeleza kule kule”

“Nimeeleza na jibu nililolipata ni kuwa nije nikubaliane na wewe”

“Tukubaliane nini?”

“Kwamba hao watu waachiwe kwa sababu mimi sijaitumia zile pesa, sasa kwanini nikae na watu wale. Nani atawahudumia?”

“Ni sawa, nimekubaliana na wewe”

“Sasa nilichoambiwa pale ni kuwa uende na wewe ukatoe uamuzi wako”

“Sawa, twende”

Maalim akatangulia kwenda kwenye ule mti. Nikamfuata.

Tulipofika kando ya ule mti, kile kivuli kilijitokeza chenyewe kikatoa sauti.

“Sasa umekuja na Maalim?”

“Ndiyo nimekuja naye kwa suala lile la mama yake na mwanawe” Aliyejibu alikuwa Maalim.

“Je mmekubaliana nini?”

“Kwamba tuwaachie kwa sababu hawatakuwa na kazi tena”

“Tuwaachie wawe wazima?”

“Nataka wawe wazima” Hapo nilijibu mimi kwa haraka bila kuulizwa.

“Mwenyewe ameshajibu” Maalim akajibu.

Pakapita ukimya wa sekunde kadhaa kabla ya ile sauti kusikika tena.

“Sasa itabidi atoe kafara mbadala ili kumkomboa mama yake na mwanawe”

“Atoe kafara gani?” Maalim akauliza.

“Atoe ng’ombe dume mweusi”

Maalim akanigeukia mimi.

“Umesikia, umeambiwa kama unataka kuwakomboa mama yako na mwanao utoe ngo’mbe dume mweusi”

“Nimtoe wapi?” nikamuuliza.

“Umtoe hapa hapa” Ile sauti ndiyo iliyojibu.

“Yaani utuletee ng’ombe mweusi kabla hujarudi kwenu” Maalim akanifafanulia.

“Utanionesha wanapouzwa. Nitanunua mmoja nimlete”

“Kama mmekubaliana mimi naondoka” Ile sauti ikatuambia na hapo hapo kile kivuli kikatoweka.

“Basi twende zetu, tumeshapata ufumbuzi” Maalim akaniambia.

Tukaondoka na Maalim. Tulipofika kwa yule mtu mwingine Maalim alimwambia.

“Asubuhi utampeleka huyu mtu akanunue ng’ombe dume mweusi, mje naye hapa”

“Sawa”

Itaendelea kesho usipitwe na uhondo huu hapahapa kumekucha.com

1 comment:

  1. NDAGU YA MALI KWA (MASHARTI) NDANI YA MASAA 72(SIKU TATU) PAPO HAPO KIKUBWA UWE MWAMINIFU, JASILI NA UWE NA UTAYARI WA KUPOKEA MASHARTI YA KUTUNZA SIRI HII SIO MZAHA......

    (HUSITUME SMS PIGA SIMU KUHEPUKA MATAPELI)

    PUUZA UONGOFU WA KUWA MTU KUWA TAJIRI NI DHAMBI WAKATI AKUAMBIAE YEYE NI TAJIRI (Tumia ufahamu kujinasuaUTAJIRI WA

    NAITWA DR, MDIRO piga 0742162843. KAMA UNAITAJI PESA ZA MAJINI AU NDAGU YA MALI AU ULINZI KWA MALI YAKO

    MATIBABU MENGINEYO NI KAMA UTULIVU KATIKA NDOA, AU KUMVUTA UMPENDAE, KUONDOA MIKOSI, MABALAA, KUOSHA NYOTA, KUITAMBUA NYOTA YAKO NA ASILI YA KAZI YAKE.
    JINI MAHABA NA SHIDA YA UZAZI. NIPIGIE 0742162843. KIKUBWA NI KUSIKILIZA NA KUFATA MASHARTI. ANGALIZO USITUME SMS PIGA NA UWE NA NIA.

    (kuhusu utajiri au pesa) KABLA YA KUPIGA SIMU ZINGATIA YAFUATAYO
    1. uwe una umri wa miaka 18+
    2. uwe tayari kupokea masharti yote
    3.uwe na uwezo wa kutunza siri
    4. uwe jasiri wa kupokea taarifa yoyote
    KARIBU SANA KWA SHIDA NYINGINE PIA ULIYONAYO AMBAYO SIJATAJA INSHAALAH ITATATULIWA IKIWA NDANI YA UWEZO WANGU.

    ReplyDelete