ILIPOISHIA
“Halafu
nitoke naye?” Herieth akamuuliza Sara.
“Toka
naye, kwani kuna tatizo gani! Atakuchuukua nyumbani kwake”
“Lakini
pesa yake haina tabu?”
“Haina
tabu kabisa. Dhamana yako ni mimi”
Saa
tatu usiku jamaa huyo akawasili. Alikuwa Njoroge. Sara akamkutanisha na Herieth,
wakayazungumza na kukubaliana kuwa usiku ule Herieth akalale kwa Njoroge.
Kutoka
saa tatu usiku Njoroge aliendelea kunywa bia hadi saa sita baa ilipofungwa.
Akaondoka na Herieth kwa teksi kuelekea nyumbani kwake.
Kutoka
siku hiyo Herieth na Njoroge wakawa wapenzi. Mapenzi yaliponoga Herieth
akahamia kwa Njoroge. Baada ya kuishi kwa mwaka mmoja wakakubaliana kuwa
wachumba.
SASA
ENDELEA
Wakati
huo Herieth hakuwa Herieth yule aliyetoka Kiambu. Alikuwa Herieth mwingine
aliyenawiri na kujisikia. Alikuwa mrembo ambaye shida ndogo ndogo zilimpitia
mbali.
Sara
alihisi kwamba Njoroge alikuwa mwanaume makini aliyeweza kutunza mwanamke
kuliko alivyokuwa akimdhania. Aliamini
kuwa yeye ndiye aliyebadili maisha ya Herieth.
Akajiambia
laiti angempata yeye angeweza kuyabadili maisha yake na kuwa bora zaidi. Akaona
kwamba alifanya kosa kumpeleka mwanaume huyo kwa rafiki yake badala ya kubaki
naye yeye.
Ndipo
alipoanza kufikiria kumnyang’anya Herieth mwanaume huyo. Alianza kwa
kumrembulia macho Njoroge na kumfanyia dhihaka za makusudi ili Njoroge amuone
kuwa alikuwa na kitu ndani ya moyo wake.
Wakati
huo Herieth hakuwa ametambua kilichokuwa ndani ya mawazo ya mwenzake.
Aliuchukulia mzaha wa Sara kwa mwanaume wake ni wa ushemeji tu.
Kulikuwa
na siku moja ambayo Herieth na Sara walikuwa kwenye mapumziko. Njoroge alifika
hapo baa na kukuta ujumbe kuwa amfuate Sara nyumbani kwake kwa vile alikuwa na
shida naye muhimu.
Kutokana
na wito huo Njoroge baada ya kupata
chupa tatu za bia alindoka akapanda matatu na kwenda nyumbani kwa Sara.
Si unajua matatu ya Kenya hususani ya Mombasa yako na misemo kila aina na utachoka wewe mwenyewe kusoma na kila moja ni zuri zaidi ya mwenzake, mie matatu niliyopanda ilikuwa na jina lililoandikwa "Mpende akupendae"
Alipoingia
chumbani kwake alikuta mambo ambayo hayakuwa ya kawaida. Juu ya meza alikuta
chupa kadhaa za bia, nyingine zikiwa tupu na nyingine zikiwa hazijanywewa.
Sara
mwenyewe alikuwa amejilaza kitandani akiwa amelewa chakari.
Siku
hiyo Sara alikuwa amemtega Njoroge. Alikuwa amevua nguo na kubaki na nguo ya
ndani halafu alilala kifudi fudi.
Njoroge
alianza kuutupia macho mwili wa Sara akiulinganisha na wa Herieth. Alianzia
kwenye miguu, akaona ilikuwa miguu ya bia. Macho yake yakapanda taratibu na kufika
kwenye magoti. Yalikuwa magoti ya mfuto.
Macho
yaliendelea kwenda. Sasa rangi ya ngozi libadilika, ilikuwa ngozi laini nyeupe kama ya mtoto mchanga. Macho yalizidi kwenda…
Mpaka
anafika kwenye kiuno Njoroge alikuwa hoi. Alimeza funda la mate akahisi mwili
ukimsisimka.
Zile
bia tatu alizokunywa zikawa zimewasha moto ndani ya mwili wake.
Akasogea
karibu na kitanda akamuwekea mkono kwenye bega na kumuita.
“Sara!
Sara!”
Sauti
ya Sara ikasikika kwa mbali ikimuitikia lakini hakuinuka wala kugeuka.
“Mbona
uko hivyo?”
“Unasema
nini…?” Sara ikamuuliza kilevi. Alikuwa
bado ameuficha uso wake kwenye mto.
“Hebu
geuka basi…umelewa kiasi hiki!”
“Nani
wewe…?”
“Mimi
Njoroge, niliambiwa unaniita”
Sara
akaugeza uso wake na kumtazama Njoroge. Macho yake yalikuwa mekundu na hayakuwa
yamefumbuka sawa sawa.
“Kaa
hapa” Sara akamwambia Njoroge katika hali ya ulevi.
“Nikae
wapi?”
“Kaa
hapa”
Sara
alimuonesha kwenye kitanda alichokuwa amelala. Njoroge akaketi pembeni mwa
kitanda. Sara akaliweka paja lake
juu ya paja la Njoroge.
“Unasema
unatoka wapi?” akamuuliza.
“Natoka
kazini kwako. Nimekuta ujumbe kuwa unaniita”
“Ndio
nilikuachia ujumbe huo. Nilitaka tuje tunwe nyumbani”
“Una
maana bia zote hizi ulikuwa unakunywa peke yako”
“Ni
chache tu. Nyingine nimekuachia wewe”
“Mbona
uko hivyo, kwanini umevua nguo?”
“Joto.
Nilikuwa nasikia joto sana.
Halafu nasikia…”
“Unasikia
nini?”
Badala
ya kumjibu Sara aliupeleka mkono wake akalipapasa tumbo la Njoroge kisha
akaushusha mkono huo taratibu huku akiendelea kupapasa....
Usaliti
wa Sara kwa Herieth ulianzia hapo. Baada ya kumtega Njoroge kama
alivyoweza kumtega alifanikiwa kumpata siku ile.
Kinyume
cha matarajio yake, Njoroge aliondoka nyumbani kwa Sara jua likiwa
limeshakuchwa.
Tangu
siku ile yeye na Herieth wakawa wanagawana penzi kwa Njoroge bila Herieth
kujua.
Siku
moja wakati Njoroge na Sara wamekaa nyumbani kwa Sara, Sara alimwambia Njoroge.
“Kwanini
huachani na yule mshamba?”
“Kwanini?”
“Sasa
wa kazi gani yule, hata halingani na hadhi yako. Huoni aibu kuwa na mwanamke kama yule?”
“Wewe
si ndiye uliyenitafutia?”
“Nilikutafutia
mbanjuke kwa siku moja tu. Naona mwenzangu sasa unataka uoe kabisa!”
“Nina
mpango huo. Nimegundua Herieth ni msichana mtulivu sana”
“Na
aende zake, ana utulivu gani, malaya mkubwa! Au ni kwa vile sijakwambia siri
zake”
“Siri
zake zipi?”
“Hebu
achana naye bwana!”
“Siwezi
kumuacha Herieth”
“Utamuacha
tu, nitahakikisha unamuacha”
Wambeya
wa pale baa walikuja wakamwambia Herieth kuwa rafiki yake alikuwa akimsaliti
kwa Njoroge. Kwanza Herieth hakuamini lakini kulikuwa na siku moja Herieth alipigiwa
simu na mmoja wa marafiki zake aliyemwambia kuwa aende nyumbani kwa Sara
akajionee mwenyewe.
Siku
hiyo Herieth alikwenda nyumbani kwa Sara kwa teksi. Aliona akipanda matatu angechelewa.
Alipofika
alikuta mlango wa chumba cha Sara ulikuwa umefungwa kwa ndani. Akabisha.
Alibisha
mara kadhaa hadi aliposikia sauti ya Sara ikitokea chumbani.
“Wewe
nani?”
Herieth
hakujibu, aliendelea kugonga tu. Hatimaye mlango ukafunguliwa. Sara akatoa
kichwa.
Herieth
akajitumbukiza ndani ghafla na kumkuta Njoroge akiwa kitandani. Alikuwa na suruali
yake lakini hakuwa na shati.
Sara
naye alikuwa amevaa khanga moja tu.
Ulikuwa
ni mshituko uliotokea mle chumbani.
Mshituko
ulianzia kwa Herieth baada ya kumkuta Njoroge akiwa kitandani chumbani kwa
rafiki yake huku rafiki mwenyewe akiwa amevaa khanga moja.
Mshituko
huo ulimkumba Njoroge baada ya kumuona
Herieth akiingia mle chumbani hali iliyodhihirisha kuwa amefumaniwa.
Sara
hakutarajia kuwa Herieth angetokea na angeingia mle chumbani kinguvu. Akawa
ameshituka kwa kukutwa na mchumba wa rafiki yake.
Akapigwa
na butwaa kwenye mlango.
“Za
mwizi ni arobaini. Leo arobaini yenu imefika, nimewafuma. Nilikuja hapa kwa
ajili ya kuwafumania nyinyi” Herieth aliwambia kwa hasira kabla ya kumtazama Sara.
“Sikutegemea
rafiki yangu kuwa ungeweza kunisaliti kiasi hiki. Asante
sana”
Njoroge
na Sara walikuwa wamenyamaza kimya. Fumanizi hilo hawakuwa wamelitegemea.
“Nawaacha
muendelee na starehe zenu lakini wewe bwana uchumba wetu unaishia hapa”
ITAENDELEA kesho usikode uhondo huu hapahapa kumekucha.com
No comments:
Post a Comment