Kumekucha blog
Pemba, WAZAZI na walezi Micheweni Wilaya ya
Kaskazini Pemba wameitaka Serikali na wadau wa elimu kukemea tabia ya makampuni
ya uchimbaji mawe na kokoto kuwaajiri watoto wadogo wenye umri wa kwenda shule
kufanya kazi za uchimbaji na ubanguaji wa kokoto.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti baada ya mwandishi wa habari hizi kuwahoji wazazi wa kijiji
cha Maziwang’ombe kuwepo kwa taarifa za watoto wao kujishughulisha na kazi za
uchimbaji wa mawe na kokoto, wamedai ugumu wa maisha umepelekea wazazi kuwacha
huru.
Walisema
watoto wengi wenye umri wa kwenda shule wamekuwa wakijishughulisha na uchimbaji
wa mawe katika migodi na kupata pesa jambo ambalo limekuwa
likiwasahaulisha umuhimu wa kwenda shule
pamoja na wazazi wao
“Tatizo la
watoto wetu kujishughulisha na kazi ya uchimbaji wa mawe na kokoto lipo zamani
na halikomeshwi---vijana wengi wamekuwa wakikatisha masomo na wengine
hawajaenda kabisa na kutojua kusoma wala kuandika” alisema Makame Shaame
“Jambo la
kushangaza ni kuona hakuna taasisi wala wadau wa elimu kuhoji watoto wadogo
kufanya kazi ya uchimbaji wa mawe na ubanguaji wa kokoto wakiamini kuwa muda
huo ni wa kuweko shule” alisema
Kwa upande
wake mkazi wa Mapofu, Ali Sheha, amewalaumu wazazi kuwaacha watoto wao
kujishughulisha na majukumu ambayo hawana ulazima nao yakiwemo ya kufanya kazi
ya kuchimba mawe na kuendesha magari ya mizigo.
Alisema
wazazi wengi wamekuwa wakiwapa majukumu watoto yakiwemo pia ya kuendesha magari ya ng’ombe
kwa ajili ya kubeba mizigo na hivyo kuwataka kuwabidiisha na masomo.
“Ni sisi
wazazi na walezi wenye kulaumiwa kwa kuwaacha vijana wetu huru na kuacha
kuwafuatilia maendelo ya masomo yao mashuleni----ndio utaona wengi wako mitaani
na barabarani” alisema Sheha
Alisema ili
kuweza kuwasaidia watoto hao ni jukumu la kila mzazi na mlezi kuhakikisha
vijana wao wanapata elimu stahiki na kuwa na utaratibu wa kuwafuatilia
maendeleo shuleni na kuwa msaada wa maisha yao ya baadae.
Mwisho
No comments:
Post a Comment