Saturday, May 14, 2016

MGAMBO JKT YAHEMA NA KUCHUNGULIA TUNDU LA SINDANO



 Madenge Ramadhani akivutwa jezi na mchezaji wa Mgambo, Salim Kipanga wakati wa mchezo ligi kuu Tanzania Bara uwanja wa Mkwakwani Leo.
KOCHA Mkuu wa Mgambo JKT, Joseph Lazaro, amesema ushindi wa bao moja kutoka kwa maafande wenzao Ruvu JKT, ni sawa na kuwapeleka Fainal hivyo kuwa na matumaini ya kubaki ligi kuu msimu ujao.
Lazaro alisema kuwa mchezo huo ulikuwa mgumu na alikuwa na presha kuanzia dakika ya kwanza kwa madai kuwa kama timu yake ingefungwa angeungana na kakaza o Coastal Union kucheza ligi ya mchangani.
Alisema timu yake iko na imani ya kusonga mbele na kubaki ligi kuu msimu ujao hivyo kuwataka washabiki na wakazi wa Mkoa wa Tanga kuiombea dua na kuiunga mkono kila ichezapo uwanjani.
Kwa upande wake Kocha wa Ruvu JKT, Abdalla Kibadeni alisema Mgambo walistahili kuondoka na pointi tatu kwani walicheza vizuri zaidi yao.
Alisema alitambua kuwa Mgambo watakuwa mbogo kwani endapo tungewafunga wangeteremka daraja hivyo safari bado ni ndefu.
Alisema kwa kipigo hicho timu yake iko katika wakati mgumu hivyo wanarudi kwao Ruvu kujipanga mpya ili mchezo wake na Simba waweze kuibuka na pointi tatu ambazo sio rahisi kwa vijana hao wa Jangwani.
.

  Mchezaji wa Ruvu JKT, Madenge Ramadhaniakiwatoka wachezaji wa Mgambo JKT wakati wa mchezo ligi kuu Tanzania Bara uwanja wa Mkwakwani leo.
  Mchezaji wa Mgambo JKT, Full Maganga akimfanyia faulo mchezaji wa Ruvu JKTMadenge Ramadhani wakati wa mchezo ligi kuu Tanzania Bara uwanja wa Mkwakwani leo.

Mchezaji wa Ruvu JKT, Paulo Mhidze  (9) akijaribu kumtoka mchezaji wa Mgambo JKT, Alli Ufudu wakati wa mchezo ligi kuu Tanzania Bara uwanja wa Mkwakwani leo.

No comments:

Post a Comment