SIMULIZI ZA FAKI A FAKI 0713 340572, 0655 340572
SITASAHAU NILIVYOGEUZWA PAKA SEHEMU YA 15
ILIPOISHIA
Jingine
nililojifunza kwa wachawi hao ni kuwa hawahurumiani wala hawana
ushirikiano.Ushirikiano wao ni kwenye uchawi tu. Kwa upande wangu niliona
nisingeweza kuendelea kuishi na watu kama hao.
Sasa
nifanye nini? nikajiuliza.
Kama
mke wangu angekubali kutoka kusingekuwa na tatizo.Tatizo ni kujitoa mimi peke
yangu. Hilo lisingewezekana. Kwa hiyo kwa ajili ya kulinda usalama wangu
niliona niendelee kuwa katika kundi hilo huku nikitafuta namna ya kuwakimbia.
Ilipofika
usiku nilimuuliza Chausiku kama mkutano wetu utakuwepo kule uwanjani.
"Kwanini
usiwepo!" akanijibu kwa sauti ya kuhamaki.
SASA ENDELEA
“Sasa hapo ndipo kwenye tabu.
Unaweza kuja kuumbuka au kuuwawa’
“Hapa kiunoni kwangu kila siku
ninavaa kamba ya mgomba, ina kihirizi kidogo. Nilitengenezewa na bibi.
Ukiona hii kamba inakukaza au kukushika ujue kuna hatari. Hapo hapo
unaondoka.”
“Sasa wale wanawake waliouawa
hawakulijua hilo?”
Huenda walivunja miko kama
alivyosema bibi. Unapokwenda sehemu unatakiwa ujiandae, sio unakwenda tu.
Halafu pia huenda walisahau kuvaa hizo kamba. Tutakapoanza kutoka
nitakuwa nimeshakutayarishia kamba yako”
“Nionyeshe pia
unavyoitayarisha na mimi nijue”
“Nitakuonyesha”
“Halafu ule uchawi wa kugeuka
mbwa au paka pia nataka kuujua’
‘Wewe hutaki kukaa na bibi
ndio maana unakosa mambo mengi. Ungekuwa unakwenda kwake mara kwa mara”
“Bibi yako simuelewi. Siku ile
naenda kumtembelea ananivulia nguo, ananiambia nipande kitandani!”
Nilipomwambia hivyo mke wangu
akaangua kicheko .
“Wewe ungemsikiliza na kufuata
anavyokuambia”
“Hata kama anataka…..?”
Chausiku badala ya kunijibu
aliendelea kucheka
“Mbona unacheka?’
“Unanichekesha. Wenzako
wanalala na maiti, wewe unamuogopa mzee?
“Siwezi, bora nife”
“Basi nitakufundisha mimi huo
uchawi wa kugeuka paka. Tutakuwa tunageuka pamoja tangu tunatoka
nyumbani”
“Nifundishe sasa hivi’
‘Ngoja nizungumze na bibi.
Wewe hujawahi kula nyama zetu”
“Nyama zipi?”
“Utazijua siku utakapokula”
“Nyama za maiti?”
“Ndio hizo hizo”
“Nyama za maiti siwezi kula”
“Tamu sana, usiiogope”
“Hapana , bora kuacha kabisa”
“Unasema nini?
Mke wangu alikuwa
ameshabadilika uso wake na kuonesha ukali. Nikamuona akifungua fundo
kwenye kaniki alilokuwa amejitanda. Akatoa kipande cha nyama. “Hii hapa ‘
akaniambia na kuitia mdomoni kwake, akawa anaitafuna.
Mwili ukanisisimka. Sikutaka
kumuliza ni maiti ya nani au ameipata wapi. Nikabaki kumtazama tu. Yeye
aliendela kutafuna kwa utulivu kama anaeitafuna mishkaki.
“Inuka twende zetu” akaniambia
huku akirambaramba vidole. “Ukila nyama hii utamu wake unausikia siku
tatu. Hata zindiko halikushiki “
Sikumjibu kitu nikachukua
jembe na kapu langu nikainuka. Tukarudi nyumbani.
Kama kawaida tuliendelea
kwenda kule kiwanjani kwa siku saba ambapo tulifanya mikutano yetu na
kujadili mambo yetu mbalimbali .
Siku moja kabla ya kumalizika
siku hizo saba tulipokutana usiku tulikwenda kufukua maiti ya mtoto
aliezikwa siku ile. Kwa mujibu wa wenzangu alikuwa mjukuu wa Yule bibi
ambaye alimtoa mhanga ili afanyiwe karamu ya wachawi.
Pamoja na ukweli huo nilihisi
pia kuwa kulikuwa na njama kati ya mke wangu na yule bibi ya kunilisha
nyama ya maiti. Baada ya mwili wa mtoto kufukuliwa kila mmoja alinyofoa
kipande chake cha nyama mbichi. Akawa anakila hapo hapo tena bila kukunja
uso kama vile anakula paja la kuku wa kukaanga.
Mimi nilinyofolewa kipande na
bibi, akaniambia ‘Kula na wewe”
“Siwezi kula’ nikamjibu”
“Lazima ule pamoja na wenzako”
“Siwezi”
“Utaweza. Kata kipande
utafune”
Nilikuwa nimeshika kile
kipande cha nyama nikikiangalia.
Usibishane na mimi,
nimekuambia kula hicho kipande cha nyama.wewe si umekubali kujiunga na
sisi.”
Bibi akaniambia huku akiwa
amenitolea macho yake yanayotisha.
JE KIJANA HUYO ATAKULA NYAMA
HIYO NA NINI KITATOKEA? USIKOSE KUTEMBELEA BLOG YAKO YA TANGA KUMEKUCHA
HAPO HAPA KESHO.
No comments:
Post a Comment