Taarifa ya Oscar Pistorius kudaiwa kujaribu kujiua akiwa gerezani
Oscar
Pistoriuos mwanariadha wa South Africa ambae alimiliki vichwa vya habari
baada ya kuhukumiwa kifungo cha miaka 6 jela kwa kosa la mauaji ya
mpenzi wake Reeva Steenkamp.
August 6
2016 iliripotiwa taarifa za Pistorius kukimbizwa hospitali baada ya
kupata majeraha kwenye mikono, taarifa zilizopatikana kwa wafungwa
wenzake ni kwamba alifanya hivyo kwa makusudi.
Taarifa
iliyoripotiwa hivi punde ni kwamba Pistorius amerejeshwa gerezani baada
ya kupata matibabu hospitalini kutokana na majeraha aliyoyapata. Msemaji
wa gereza alisema majeraha hayo yalikuwa ‘madogo’ na kwamba amerudishwa
gerezani.
Aidha
msemaji wa gereza ameongeza kuwa Pistorius amekanusha taarifa
zilizotolewa kuwa amefanya hivyo kwa kukusudia na kuwa alitaka kujiua.
No comments:
Post a Comment