Jiji la Kisasa linajengwa Marekani lakini hatoruhusiwa mtu yoyote kuishi..
Katika Jiji la New Mexico Marekani,
sehemu kubwa sana ya eneo la Jiji hilo ni Jangwa na Milima mikubwa… ni
eneo kame kabisa ambalo sio rahisi mtu akavutiwa kuishi.
Wataalam wa Masuala ya Teknolojia wamekuja na hii mpya , hapohapo New Mexico linajengwa Jiji la Kisasa.
Hilo eneo litakuwa na kila kitu kama
Jiji ambalo lina makazi ya watu, ikiwemo mitaa ya kisasa na iliyopangika
vizuri, nyumba, sehemu za hifadhi, maduka na malls kubwa.
Hii ni ramani inayoonesha Jiji la CITE litakavyokuwa.
Jiji litaitwa ‘The CITE (Center for Innovation, Testing and Evaluation)’, lakini hakuna mtu hata mmoja ambayo atabahatika kuishi hapo kwa sababu Jiji limeandaliwa kwa matumizi maalum kabisa !!
Ramani nyingine ya muonekano kutoka juu.
Kazi ikikamilika mwaka 2018 hili eneo
litakuwa na matumizi mengi ikiwemo kufanyika majaribio ya Teknolojia
mpya ikiwemo mifumo ya ujenzi wa Barabara, Majengo, Mawasiliano na
Ulinzi.
Moja ya majaribio ambayo wanapanga kuwa yawe yanafanyika huku ni kama hii ya kujaribu magari yasiyo ya madereva.
Kwa sababu hakuna binadamu atakayeruhusiwa kuishi huku, hata Helicopter zitakazotumika zitakuwa ni Drones ambazo hazina marubani.
CITE Campus, hapo patakuwa sehemu maalum watakapokuwa wanafikia watu wanaokuja kwa ajili ya kufanya Tafiti kwenye eneo hilo.
Huu ndio muundo wa nyumba zitakazokuwepo eneo hilo, kila kitu kinafanya kazi kwa kuunganishwa na Internet.
Unaweza kucheki pia story yote kwenye kipande cha Video.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment