Mazungumzo
yamekuwa yakifanyika na washauri wa kocha huyo mwenye umri wa miaka 48
tangu Jumapili na Liverpool wanajiamini mno kwamba watampata kocha huyo
wa zamani wa Borussia Dortmund.
Mkataba
bado haujasainiwa, lakini inatarajiwa kwamba Klopp atapewa mkataba wa miaka mitatu na kampuni ya Fenway Sports Group, wamiliki wa Liverpool
kama ambavyo walifanya kwa watangulizi wake, Kenny Dalglish na Brendan
Rodgers.
Klopp
amekuwa kwenye rada za FSG ili achukua nafasi ya Rodgers a mipango
imekuwa ikipelekwa haraka haraka kuhakikisha hawapotezi fursa ya kumpata
kocha huyo mwenye hadhi ya juu katika mchezo huo Ulaya.
Anatarajiwa
kuwachukua Wasaidizi wake wa muda mrefu, Zelkjo Buvac na Peter Krawietz
akafanye nao kazi, ingawa bado mustakabali wa Sean O'Driscoll, Gary
McAllister na Pepijn Lijnders, ambao wote waliteuliwa na Rodgers
haujajulikana.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment