Thursday, October 8, 2015

KOREA KUSINI WAJA NA KALI YA MWAKA

Wafanyakazi Korea Kusini wamekuja na hii ya kulipia usingizi muda wa kazi…

Korea Kusini ni moja ya Mataifa yaliyoendelea kiuchumi na raia wake hutumia masaa mengi zaidi kufanya kazi.
Utafiti uliofanywa na Shirikisho la Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo OECD ulifanya uchunguzi na kugundua raia wa Korea Kusini hufanya kazi saa 2,163 kwa mwaka tofauti na raia wa Ujerumani ambao hutumia saa 1,388.
Kilichonifikia ni kwamba wafanyakazi katika ofisi mbalimbali katika mji mkuu wa nchini hiyo Seoul wamekuwa wakilipia pesa ya usingizi wakati wakipata chakula cha mchana ili kupunguza uchovu.
duuu
Moja ya majengo yaliyopo katika jiji la Seoul
Kuna vyumba maalum kabisa vya kupumzika na hata kufanya massage ambavyo vimekuwa maarufu sana hasa katikati ya miji yenye ofisi nyingi.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment