Monday, October 5, 2015

MAAAJABU NA KWELI

Hili sio basi la abiria, ni nyumba ya kuishi inayotembea… ndani ina kila kitu muhimu..

Maisha popote… inavutia kuona ubunifu na Teknolojia vinatuletea vitu vipyavipya Duniani… Pesa yako ndio inaamua wapi uishi, wapo wenye nazo ambao watavutiwa kuwa na maisha yao ndani ya hii gari ya kifahari !!
Brand Pages-American Coach-American Eagle-Images-gal_AE_ext1
Ukiliangalia kwa nje ni basi la kawaida tu kama ambayo tumeona wasanii wengi wa Marekani wanayatumia kwenye safari zao.. lakini hili sio tour bus, hili ni Mjengo ambao ndani yake kuna mahitaji muhimu yote ambayo yanatakiwa yawepo kwenye nyumba ya kuishi, kwa maana nyingine hii ni nyumba inayotembea.
Unaweza kucheki nje mpaka ndani jinsi kulivyo kwenye hizi pichaz za Basi la American Eagle RV.
Bus V
Hili Basi likipaki, unaweza kulifanya liwe na muonekano huu ili kuongezea ukubwa wa ndani, maisha yanaendelea.
tumblr_inline_nvlpnaw3rf1tdmu50_1280
Bus II
Hapo ni ndani ya chumba cha kulala, ni humo humo ndani ya Basi.
Bus III
Muonekano wa sebule ndio huu !!
Bus VII
Hizi ni mashine za kufulia nguo.. zimo humo humo ndani ya basi.
   Bus VI Bus VIII Bus
Gharama ya kulipata hili Basi ni Dola 219,450 ambazo zinagusa mpaka Tshs. Milioni  473.

No comments:

Post a Comment