Friday, October 9, 2015

MANNY PACQUIAO ATAKA PAMBANO MOJA ATIMKIE SIASA

Pacquiao kupigana mara ya mwisho


Bondia raia wa Ufilipino Manny Pacquiao amesema kuwa kuna uwezekano mkubwa akastaafu katika ulingo wa ndondi na kutaka pambano moja tu.
Pacquiao,ambaye alipoteza kwa Floyd Mayweather katika pambano la mwisho ,anataka kuwania kiti kimoja katika bunge la seneti mwaka 2016.
Raia wa Uingereza Amir Khan amekuwa akitajwa kuwa ni mmoja ya wapinzani wa Pacquiao mwenye umri wa miaka 36,huku Terence Crwaford kutoka Marekani akiwa mpinzani mwengine.

Pacquiao amesema kuwa ''hawezi kusema'' iwapo pigano lake la mwisho litakuwa dhidi ya Mayweather,baada ya raia huyo wa Marekani kuahidi kustaafu baada ya ushindi wake dhidi ya Andre Berto.
Raia huyo wa Ufilipino ,ambaye alifanyiwa upasuaji katika bega lake baada ya pigano lake na Mayweather,anajivunia rekodi ya mapigano 57,kushindwa mara 6 na sare ya mapigano 2.

No comments:

Post a Comment