Kiungo
mjerumani Bastian Schweinsteiger ameongeza idadi ya majeruhi kwenye
klabu ya Manchester United hivi sasa baada ya kuumia jana mazoezini
akiwa na timu yake ya taifa.
Nahodha
huyo wa ujerumani, (31) alishindwa kuiwakilisha timu yake ya taifa
katika mchezo wa makundi wa kufuzu kucheza fainali za mataifa ya ulaya
EURO 2016 baada ya kuumia ankle dakika chache akijiandaa na mazoezi.
Bastian
anaungana na nahodha wa Manchester United na England, Wayne Rooney
ambaye naye atakosa michezo miwili itakayochezwa na England leo Ijumaa
na wiki ijayo kwa kuwa majeruhi.
United
pia iko katika hali mbaya baada ya mlinzi wake muargentina Marcos Rojo
naye kutokua fit kucheza na hatimaye akaenguliwa katika kikosi cha timu
ya taifa ya Argentina.
Bado
haijafahamika kama wachezaji hao watakua fit tayari kuiwakilisha United
katika mchezo mgumu dhidi ya Everton weekend ijayo ya tarehe 17
October.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment