Pilipili huchangia maisha marefu,Utafiti
Kwa miaka mingi
sasa, binadamu amekuwa akitumia pilipili kuongeza ladha kwenye mlo wake.
Kuna wanaovutiwa na ukali wake na vilevile wanaoichukia kutokana na
ukali huo.
Sasa utafiti umeonyesha si ladha tu ambayo pilipili huongeza, bali pia hufanya wanaoila kuwa na maisha marefu.Matokeo ya utafiti yaliyochapishwa kwenye jarida moja la matibabu nchini Uingereza kwa jina British Medical Journal yanasema kula mlo uliotiwa viungo, ikiwemo pilipili, huwa na manufaa kwa afya ya binadamu.
Wanasayanasi kutoka Uchina waliangazia afya ya watu takriban laki tano waliojitolea kushirikishwa katika utafiti kuhusu manufaa ya pipili kwa muda wa miaka kadhaa.
Matokeo ya uchunguzi huo yamebaini kuwa wahusika waliokula chakula kilichokuwa na wingi wa viungo, mara moja ama mara mbili kwa wiki walipunguza hatari yao ya kufa kwa asilimia 10.
Viwango vya hatari ya kufariki pia vilionekana kupungua kwa kiasi kikubwa kwa waliokula vyakula vilivyotiwa vikolezo kwa wingi kila siku.
Katika uchunguzi huo, sehemu kubwa ya viungo kwenye chakula ilikuwa pilipili, na kwa waliokula pipili mbichi walionekana kupunguza hatari ya kufariki kutokana na saratani, ugonjwa wa kisukari na pia maradhi ya moyo.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment