Mshambuliaji wa Chelsea, Eden Hazard (kushoto) akifumua shuti la nguvu kuisawazishia timu yake usiku wa jana katika mchezo wa Ligi Kuu ya England dhidi ya Tottenham Hotspur Uwanja wa Stamford Bridge, London timu hizo zikitoka sare ya 2-2. Bao lingine la Chelsea limefungwa na Gary Cahill, wakati ya Spurs yamefungwa na Harry Kane na Son Heung-min na kwa sare hiyo Leicester City wanakuwa mabingwa wapya wa England kwani pointi zao 77 haziwezi tena kufikiwa na Spurs.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa Tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment