DAMPO la Duga kata ya Mabawa Tanga, likiwa limefurika takataka (Uchafu) uliozagaa hadi katika makazi ya watu na kuzusha taharuki kipindi hiki cha magonjwa ya miripuko na baadhi ya familia kuhamisha watoto wao kuepuka magonjwa.
Dampo hilo kwa sasa limekuwa hatari kwani linaelekea katika makazi ya watu baada ya eneo lililotengwa kujaa hivyo kuzaliana wadudu hatari na nyoka wakali.
Baadhi ya familia ambazo ziko kandokando na Dampo hilo wameiambia tangakumekuchablog kuwa kwa sasa hali ni mbaya hivyo kuhitajika kuchukuliwa hatua za dharura kuepusha majanga.
Wamesema kama halmashauri ya jiji wangelikuwa na utaratibu wa kuchoma takataka na kuhakikisha dampo hilo halisogei katika makazi ya watu kitisho hicho kisingekuwepo na familia kuhama.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog, blog ya habari za papo hapo
No comments:
Post a Comment